Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum akiwa katika picha ya pamoja
wafanyabiashara alipotoa Taarifa ya muafaka uliofikiwa kati ya
wafanyabiashara na serikali juu ya Matumizi ya Mashine za kielektroniki
(EFDs) leo Jijini Dar es Salaam, Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya
wafanyabishara Bw. Johnson Minja na Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi
ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mzee Benard Mchovu
(Picha na Regnihaldah Mpete-TRA)
Na Anitha Jonas – MAELEZO.
Serikali yafikia muafaka katika mgogoro wake na wafanyabiashara juu ya
matumizi ya mashine za kieletroniniki EFD’s.
Hayo ameyasema leo Waziri wa Fedha Mhe.Saada Mkuya alipokuwa akitoa
taarifa hiyo kwa vyombo vya habari juu ya Serikali kufikia muafaka wa
makubaliano yaliyofanyika kwa ushirikiano wa Kamati kuu ya Taifa iliyoshirikisha
wajumbe kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Viongozi wa Jumuiya
ya wafanyabiashara katika ngazi ya Taifa.
“Matumizi ya mashine za EFD yalipoanza yalileta changamoto kwa
wafanyabiashara ,hivyo niliunda kamati ya kitaifa pamoja na kamati katika ngazi
za Mikoa na Wilaya pamoja na wenyeviti wakuu wa mikoa kutafuta suluhu la
suala hili”alisema Mhe. Mkuya.
Waziri Mkuya aliendelea kusema Kamati imetoa mapendekezo mbalimbali kwa
Serikali ikiwemo ya muda mfupi ambayo wameshaanza kuyafanyia kazi na
mengine ni yakisera ambayo yatahitaji muda mrefu yatafuata utaratibu
unaopaswa katika utekelezaji wake,kwa ufuatiliaji na ushirikiano wa karibu,kupitia
kamati ya Kitaifa itakayodumu kwa kipindi cha miaka miwili.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini Bw.Johnson Minja
aliipongeza serikali kwa kubali kukaa meza moja na wafanyabiashara katika
kutatua mgogoro huo uliyokuwepo katika matumizi ya mashine za EFD na
kuakukubali kupokea changamoto za wafanyabiashara na kuahidi kuzifanyia kazi.
“Serikali imekubali kupitia mfumo wa utozwaji kodi kuanzia ngazi ya bandarini na
kuongeza uwazi ilikuleta uelewa kwa wafanyabiashara na kuepuka kutozwa kodi
kubwa kutoka na kukosa uelewa wa gharama za ulipaji kodi”,alisema Bw.Minja.
Aidha Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ya wafanyabiashara aliendelea kusema ni
wajibu wa kila mmoja kulipa kodi na hii ni kwa maendeleo ya nchi na pia ni kosa
kwa mfanyabiashara yoyote kuendesha biashara yake bila kuwa na namba ya
utambulisho wa mlipakodi (Tin Number),tunataka namba ya walipakodi iendelee
kuongezeka na kuondoa kabisa wafanyabiashara wasio lipa kodi.
Mbali na hayo nae Kamishana Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Rished Bade
aliipongeza kamati kwa kuweza kufika mwafaka na kuweza kuzitambua
changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwasumbua wafanyabiashara na ameahidi
,kuwa ofisi yake itaendelea kuwawajibisha watu wote wanao kiuka taratibu za
ulipaji kodi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...