Benki
ya NMB imedhamini mkutano mkuu wa Mwaka wa Makanda wa Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji Tanzania bara ulioanza leo mkoani Mororogoro.
Katika
mkutano huo, NMB imeweka mabanda ya maonyesho yanayotoa elimu juu ya
huduma mbalimbali zinazopatikana ndani ya benki ya NMB pamoja na
kutoa huduma za papo kwa papo ambapo wajumbe wa mkutano huo walipata
wasaa wa kufungua akaunti za chap chap pamoja na kupata huduma za NMB
Wakala.
Kwa huduma za NMB Wakala, wateja wa NMB wanaweza kutoa na kuweka
fedha kwenye akaunti zao za NMB bila ya kwenda
kwenye tawi lolote la NMB.
Mkutano huo ulioanza leo, utafanyika kwa siku tano mpaka Ijumaa ya Tarehe 5, Juni, 2015.
Kamishna
jenerali wa jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania bara - Pius Nyambacha
akimsikiliza mfanyakazi wa benki ya NMB - Nehemiah Simba na
akifafanua jambo wakati akieleza namna ya huduma ya kufungua akaunti ya
NMB chapchap Instant account mara baada ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa
mwaka wa makanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji Tanzania bara
uliofanyika mkoani Morogoro leo.
Meneja wa
NMB kanda ya mashariki - Nazareth Lebbi akielezea jambo kwa Naibu
Kamishna wa Utawala na Fedha jeshi la zimamoto na uokoaji - Billy
Mwakatage na Mwakilishi wa mkuu wa wWilaya ya Morogoro - Ester
Rugaira wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa makanda wa jeshi hilo mkoani
Morogoro.
Meneja wa
NMB kanda ya mashariki - Nazareth Lebbi akizungumza jambo na Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani - Mwamini
Malemi wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa makanda wa jeshi
la zimamoto na uokoaji Tanzania bara uliofanyika mkoani Morogoro leo.
katikati ni Kamishna jenerali wa jeshi hilo - Pius Nyambacha.
Kamishna
Jenerali wa jeshi la zimamoto na uokoaji Tanzania bara - Pius Nyambacha
akizungumza jambo na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa jeshi
la Magereza - Dkt Kato Rugainunura wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa
makanda wa jeshi hilo mkoani Morogoro. kulia ni Meneja wa NMB kanda ya
mashariki - Nazareth Lebbi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...