mazingira 3Mchambuzi wa mambo ya mazingira katika ukanda wa bahari na mwandishi mwandamizi wa habari nchini Kenya, Wanjohi Kabukuru, akielezea jambokwa wandishi wa habari (hawapo pichani) katika warsha hiyo juu ya 
mazingira

Na Andrew Chale, Nairobi, Kenya
Wataalamu wa kichunguzi na wanasayansi wa Mazingira, wameelezea kuwa visiwa vilivyopo ndani ya bahari ya Hindi vinatarajiwa kutoweka duniani kutokana na mabadiriko ya tabia nchi inayoikumba dunia kwa sasa ikiwemo upungufu wa kimo cha bahari, ukame na hali ya joto sehemu mbalimbali duniani.

Hayo yameelezwa jijini hapa katika mafunzo juu ya kuripoti habari za mazingira na mabadiriko ya tabia nchi (Climate Change) mafunzo yaliyoanza jana Juni 1, 201a5 ambayo ni maalum kwa wandishi wa habari wanaoandika katika mitandao ya kijamii blog na tovuti kutoka nchi mbalimbali za Afrika, zikiwemo Tanzania, Rwanda, Madagasca, Kenya na Ufaransa ambaoyo ni ya wiki mbili ambao pia ni mkutano wa maandalizi kuelekea katika kongamano la mazingira litakalofanyika jiji la Paris, Ufaransa, Julai na Desemba mwaka huu.

Akielezea hali hiyo, Mchambuzi wa mambo ya mazingira katika ukanda wa bahari na mwandishi mwandamizi wa habari nchini Kenya, Wanjohi Kabukuru, alibainisha kuwa, visiwa vingi ndani ya bahari ya Hindi ikiwemo Mombasa, Comoro na Madagasca vimo hatarini kutoweka kabisa duniani kutokana na tabia nchi (Climate Change).

“Utafiti mbalimbali umefanyika na kutokana na mabadiliko ya tabia nchi Dunia itaingia katika matatizo makubwa. Hasa kwa upande wa bahari ardhi iliyo ndani yake kuja kumezwa ikiwemo visiwa vya Zanzibar, Madaga” alieleza Kabukuru ambaye pia ni mchambuzi na mtafiti wa masuala ya mazingira ya ukanda wa bahari anayefanya kazi zake nchini Kenya.

Kwa Tanzania tayari athari mbalimbali zimeanza kujitokeza kutokana na tabia nchi ambapo kwa sasa mmomonyomko wa radhi umeweza kukumba maeneo zaidi ya 148 ambayo yanaingia maji ya chumvi huku wakulima wakishindwa kuendelea na kilimo cha kawaida.

Mkutano huo ulioanza leo Juni Mosi, umeandaliwa na Media Coperation CFI kutoka nchini Ufaransa ulio na lengo la kutafuta njia mbadala juu ya kuripoti habari za mabadiliko ya tabia nchi kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Ufaransa Kenya na shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), kwa washiriki wa Tanzania,wanawakilishwa na Andrew Chale mtandao wa modewjiblog na Dotto Kahindi mwandishi wa habari wa kujitegemea.
mazingira2Wanahabari wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na Mchambuzi wa mambo ya mazingira katika ukanda wa bahari na mwandishi mwandamizi wa habari nchini Kenya, Wanjohi Kabukuru (Hayupo pichani) mafunzo hayo yanaendelea jijini Nairobi hadi Juni 11, mwaka huu.
DSC_0466Mwakilishi anayeiwakilisha Tanzania, Mwandishi mwandamizi wa mtandao wa MODEWJIBLOG.COM, Andrew Chale (kulia) akiwa katika mkutano huo... unaoendelea katika jiji la Nairobi.
wwwAfisa wa CFI, kutoka Paris, Ufaransa, Anne-Sophie Ricco akielezea jambo juu ya mkutano huo kwa wandishi wa habari wa tovuti na blog (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa mikutano wa Safari Club, Jijini Nairobi, Kenya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 02, 2015

    Kama ndio kusudio lenu kuiondoa ZANZIBAR kwenye map ya dunia , hamtowahi , hiyo climate change itaanza huko kwenu mount kilimanjaro itakapo erupt kwani tushaona milima iliyokuwa un active volcano ime erupt after 50 yrs

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 03, 2015

    Nina wasiwasi na elimu yako wewe anon hapo juu, unaonekana huelewi unachoongea zaidi ya kutoa uchafu wako mdomoni. Unabishi climate change wakati ni kitu kilicho wazi, Kuna visiwa vingi vilivyozama kutokana na kina cha habari kuwa juu kutokana na kuyeyuka kwa barafu,Zanzibar na sehemu nyingine za pwani zipo chini ya meta za usawa wa bahari 0 (0.0 A.S.L) na kuna ushahidi hivi visiwa vinalika kwa kasi kubwa, ina maana hujui kuwa sehemu ya kisiwa cha unguja kimeanza kuchimbika na maji ya chumvi yanachanganyika na maji yasiyo ya chumvi? (si mimi nasema hayo ila ni habari walizoongea jana baraza la wawakilishi), Sasa unavyopanua domo lako kuongea kashfa sijui Kilimanjaro italipuka....mbona hilo kila mmoja analijua? Zungumzia hicho kilichosemwa siyo mambo ambayo hayakuzungumza hapa (Mambo ya Milima, volkeno, barafu kupungua yangezungumzwa hapa isingekuwa taabu,tungetoa comment zetu) Wewe unakurupuka ndiyo maana nasema nina wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...