Maranyingi wafanya biashara hufikiria kutangaza biashara zao magazetini, kwenye mabango, vipeperushi na kadhalika. Wafanyabiashra huamini kwamba njia hizi hufikia watu wengi. Je ni kweli kwamba matangazo ya karatasi hufikia walengwa wengi? Kama mfanyabiashara na mtangazaji, unajuaje kuwa tangazo lako limefikia walengwa wangapi na kwa wakati gani?
Kwa kutumia tovuti, unaweza kujua ni watu wangapi wanao tembelea tovuti yako, na wanatembelea kwa muda gani. Kwa kujua ni watu wangapi wanaotembelea tovuti yako, utaweza kujua pia ni watu wangapi nje ya mkoa na nchi wanaopata ujumbe wa biashara yako. Kwa kujua kwa muda gani walitembelea tovuti yako, utaweza kujua kwamba ni watu wangapi waliovutiwa na biashara yako.
Hasara ya kutumia matangazo ya karatasi ni kwamba ukomo wa maisha yake ni mfupi. Siku ikiisha tu, gazeti hilo na matangazo yaliyopo ndani yanakua hayana umuhimu. Matangazo ya bandiko pia hua na maisha mafupi. Mvua ikinyesha, karatasi yako inaloana. Mtu anaweza pia akaibandua, au hata kuweka bandiko ya biashara yake juu ya lakwako.
TzNIC ni kampuni ya kiTanzania ambayo imerahisisha usajili wa tovuti za kibiashara na za kibinafsi. Kusajili tovuti yako kwa bei rahisi, sajili jina la kampuni au biashara yako au hata kama ni mtu binafsi kabla mpinzani wako kibiashara hajasajili! Kwa maelezo Zaidi tembelea kurasa za TzNic hapa chini
Website; http://www.tznic.or.tz/
Facebook; https://www.facebook.com/tznic
Twitter; https://twitter.com/tznic
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...