Ukiwa ndani ya kiota hiki ni kama uko nje ya jiji la Dar es salaam. Yaani unasahau kabisa kama kuna kelele za watu na magari duniani. Ni sauti za ndege wazuri wa angani tuu ndio zinaburudisha masikio na macho … kelele na honi za boda boda na magari hazikuhusu kabisa. Mandhari yake ni kama uko mkoa Fulani wenye baridi kali na mvua nyingi, umaridadi wa garden yake utakufanya ujione kama uko mkoa kama Mbeya ama Iringa vile! Ni kijani tupu… unaweza tamani uvue viatu na ukae chini badala ya kiti. 
Posto Bella iko kwenye Miinuko ya Bunju A, 1.2km kutoka barabara ya lami ya Bagamoyo, ambayo inapokea upepo mwanana unaotoka Bahari ya Hindi (see breeze). Baridi inayosababishwa na upepo huo ndio inayokufanya ujisikie uko ndani ya Mbeya.

Basi kwa wale marafiki wa kazini ambao mnatafuta sehemu ya kwenda kula batta zenu kwa rakhaa zenu Sehemu hii ndio maalum kabisa. Unaweza kupiga simu ukafanya maandalizi kabisa ya nini unataka uandaliwe kwa uhakika zaidi. Vinywaji vyote ni bei ya kawaida tuu.

Kwa sherehe ndogo ndogo kama kitchen parties, birthdays, corporate parties, meetings, vikao vya harusi, engagement parties, Posto Bella wanakupa garden yao for free! Yaani bure kabisa!  Mpambaji, chakula, Music ni juu yako. Unajiletea chaguo lako mwenyewe, …. Mungu akupe nini tena, kufanya sherehe yako kwenye Royal Garden hii bure na kujichagulia service providers wako.
Kwa wale wanafamilia, Posto Bella ni sehemu nzuri ya kula chakula cha mchana kutoka kwenye menu yetu. Wale wenye mikutano ya kifamilia (family gatherings) ambayo inahitaji utulivu, Posto Bella ni sehemu pekee inayokupa maximum privacy!

Please Follow us on Instagram; @posto_bella and Facebook: www.facebook.com/PostoBellaResort utapata matukio yetu ya kila wiki.

Karibu sana. Contact Us: +255 655 123695 or postobellaresort@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...