Sehemu ya ujenzi wa barabara ya Kyaka-Bugene inayojengwa wilayani Karagwe,yenye urefu wa Km 59.9 kwa mujibu wa Mkandarasi wa barabara hiyo alieleza kuwa mpaka kukamilika mnamo Desemba mwaka huu itakuwa imetumia kiasi cha shilingi bilioni 65 na ushehe. 
  Makandarasi wa kampuni ya kichina ya CHICCO, inayojenga barabara ya Kyaka-Bugene wilayani Karagwe, wakisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aliyekwenda kukagua ujenzi huo eneo la Mugulakorongo, Ndama.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa ameongozana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana wakielekea kukagua na kushiriki ujenzi wa Kiwanda cha Kahawa na Maharaga cha KADRESS,eneo la Ndama, wilayani Karagwe, Kagera.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akishiriki ujenzi wa kiwanda cha kahawa na maharage katika kijiji cha Ndama,wilayani Karagwe. Ndugu Kinana akiwa emeambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye wapo kwenye ziara ya kikazi ya Mikoa ya Kagera,Geita na Mwanza yenye lengo la kuhimiza uhai wa chama cha CCM,kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali pamoja na kusikiliza matatizo ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akisoa orodha ya vijiji vitakavyonufaika na mradi wa usambazaji wa umeme vijijini REA,mbele ya Wananchi wa Kijiji cha Nyakaiga, Kibondo, wilayani Karagwe.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akisisitiza jambo kwa wananchi  katika Kijiji cha Nyakaiga, Kibondo, wilayani  Karagwe,alipokuwa akuhutubia na kuwapiga vijembe wapinzani kwamba kamwe hawataweza kushinda uchaguzi mkuu na kuingia Ikulu kwa sababu CCM imejipanga vyema kuhakikisha inaibuka na ushindi wa kishindo.
 Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Gozibeth Blandes akihutubia katika mkutano huo
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akihutubia wananchi katika Mji wa Katanga, Makao Makuu ya Wilaya ya Karagwe, mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiapata maelezo mafupi kutka kwa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera alipotoka kukagua mitambo ya kusukuma maji kwa ajili ya umwagiliaji katika mashamba ya miwa.Pichani kushoyto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.John Mongella.

PICHA NA MICHUZI JR-KARAGWE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 12, 2015

    Tunashukuru kutujjengea barabara ya lami ya Karagwe, tuliingoja tika uhuru, tukapatiwa barabara mpaka Kyaka ikasaidia kupunguza masaa ya kufika Bukoba, sasa hivi kazi hii iliyofanyika na inayoendelea kufanyika mpaka Omurushaka imerahisisha usafiri Karagwe. Kwa hili wananchi wa Karagwe tunaipongeza serikali ya awamu ya nne na kuipigia makofi mazito. Mmefanya jambo la maana kujenga barabara hii itakayochochea maendeleo...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...