Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Albino kitaifa yatayofanyika Juni 13,mwaka huu kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo,Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Felix Ntibenda alisema wamepata fursa ya kuwa wenyeji kutokana na kutokua na matukio ya ukatili wa watu wenye ulemavu wa ngozi kutokana na takwimu za mkoa wapo Albino 199.

“Mkoa  una jumla ya watu wenye ulemavu wa ngozi wapatao 199,wakiwemo wananwake 110 na wanaume 89,hadi sasa hakuna kitendo chochote cha kikatili kilichowahi kutokea kwa Albino yeyote hapa mkoani na hivyo kuipa sifa mkoa wetu kuwa mwenyeji wa maadhimisho haya,”alisema Ntibenda

Hata hivyo alikiri kuwa taswira na ramani ya nchi imetiwa doa kimataifa kutokana na mauaji yanayoendelea katika mikoa mbalimbali nchini inakadiriwa watu wenye ulemavu wa ngozi 74 wameuawa na watu wenye imani potofu za kutumia viungo vyao kupata utajiri na mvuto kisiasa.

Ntibenda alisema jumla  ya Albino 59 wamenusurika vifo huku  11 wakipewa ulemavu wa kudumu jambo ambalo serikali ikishirikiana na wadau wengine wameamua kusimama pamoja kupinga mauaji ya kinyama kwani kila mtu kila mtu ana haki ya kuishi.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Felix Ntibenda akizungumza na waandishi wa habari leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 10, 2015

    10 years on. Govt and president haja'solve issue ya mauaji ya albino, sasa anakuja kuwaambia nini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...