Na. Catherine Sungura, MOHSW-Arusha
Zaidi ya wagonjwa elfu arobaini wanaougua ugonjwa wa vikope unaotokana na trakoma
wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa macho katika mikoa sita nchini Tanzania kwa muda wa
miaka mitano.
Hayo yamezungumzwa jana jijini hapa na Mratibu wa Mpango wa kudhibiti magonjwa
yaliyokuwa hayapewi kipaumbele dkt. Upendo Mwingira wakati akiwasilisha mada kwenye
mkutano wa nne wa kazi kati ya wizara na wadau wanaofadhili mpango huo
Upasuaji huo unafadhiliwa na shirika la msaada la Uingereza (DFID) pamoja na mfuko wa
msaada wa Malkia Elizabeth (QETF) katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Arusha, Manyara, Pwani
pamoja na Dodoma.

Dkt. Mwingira alisema tathimini iliyofanyika nchi nzima inakadiriwa kuwa na wagonjwa wa
vikope wapatao laki moja, hivyo ili kudhibiti ongezeko la upofu nchini ,serikali imeanza kufanya
upasuaji wa wagonjwa hao.
“Watu wenye matatizo ya vikope hupata usumbufu wakati kope zikigusa kioo cha jicho na
mwishowe kupofuka,hivyo njia hii ya upasuaji itawasaidia kurudi katika hali ya kawaida na
kujisaidia katika shughuli zao binafsi na zile za maendeleo ya Taifa kwa ujumla” alisema
Ugonjwa wa vikope husababishwa na bakteria aina ya “Chlamydia Trachomatis”
wanaosambazwa na inzi na pia kwa njia ya kuchangia taulo au vitambaa na kugusa macho ya
mtu anayeugua ugonjwa huo , hivyo usipotibiwa mapema unaweza kusababisha upofu.
Mkutano huo unawajumlisha wadau kutoka nchini Washington DC, Liverpool, Geneva pamoja
na baadhi ya waratibu wa mpango huo toka mikoa ya Tanzania bara.
Dkt.Upendo Mwingira akimkabidhi zawadi ya kinyago mwakilishi mkazi wa shirika la IMA World Health Jim Cox anayemaliza muda wake nchini.IMA World Health ni moja ya wadau wa mpango huo.
Dkt. Jeremiah Ngondi kutoka RTI International ambayo inatekeleza Mpango wa Taifa Kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele, akizungumza katika Mkutano huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...