Mhe. Augustine Mwarija- Jaji Mteule wa Mahakama ya Rufani,Ikulu jijini Dar es salaam Juni 16, 2015. Kabla ya Uteuzi wake Mhe. Mwarija alikuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu- Divisheni ya Biashara, anayeshuhudia pembeni ni Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania.
Mhe. Augustine Mwarija, Jaji Mteule wa Mahakama ya Rufani akitia sahihi hati ya kiapo mara baada ya kuapishwa rasmi na Mhe. Rais kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe. Stella Mugasha- Jaji Mteule wa Mahakama ya Rufani, Ikulu jijini Dar es salaam Juni 16, 2015. Kabla ya uteuzi wake Mhe. Jaji Mugasha alikuwa Jaji Mfawidhi Mahakama kuu- Kanda ya Dar es Salaam.
Mhe. Jaji Mugasha akitia sahihi hati ya kiapo mara baada ya kuapishwa rasmi na Mhe. Rais mapema leo.
Wakiongea na Waandishi wa Habari waheshimiwa Majaji hao wateule wameahidi kufanya kazi kwa bidii na kusaidia katika kuendeleza mapambano ya kumaliza mashauri ya muda mrefu.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania).







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...