Meneja Mkuu wa Mauzo ,Wateja Wadogo na Wakubwa wa Benki ya DCB,Haika Machaku ,akizungumza na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa filamu iitwayo Hamu ya Mafanikio itakayozinduliwa siku ya Jumamosi,25 June 2015 katika ukumbi wa Cinema wa Dar Free Zone.Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CONSNET GROUP LTD,Sanctus Mtsimbe.
Mkurugenzi Mtendaji wa CONSNET GROUP LTD,Sanctus Mtsimbe akizungumza na Waandishi wa Habari juu wa uzinduzi wa filamu hiyo siku ya Jumamosi,25 June 2015 katika ukumbi wa Cinema wa Dar Free Zone,kulia ni mwigizaji wa filamu hiyo,Mrisho Zimbwe(Tito)
Wawakilishi wa Benki ya DCB na Mwakilishi kutoka CONSNET GROUP LTD pamoja na Waandishi wa Habari wakisikiliza maswali yaliyokuwa yanaulizwa yaliohusu uzinduzi wa filamu iitwayo Hamu ya Mafanikio itakayozinduliwa siku ya Jumamosi,25 June 2015 katika ukumbi wa Cinema wa Dar Free Zone.
Na Bakari Issa Madjeshi
Rais Mstaafu,Benjamini Mkapa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Filamu ya Desire to Succeed ‘Hamu ya Mafanikio’uzinduzi wa filamu hiyo utaofanyika katika ukumbi wa Cinema wa Dar Free Zone Juni 25 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Hayo yalisemwa na Meneja Mauzo,wateja wadogo na wakubwa wa Benki ya DCB,Haika Machaku wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana alisema kuwa DCB wameamua kuandaa Filamu hiyo baada ya kutambua kuwa Watanzania wengi wanapenda kuangalia filamu za Kiswahili na hivyo wanaamini kuwa itaweza kuwafikia watu wengi na kufikisha ujumbe kirahisi zaidi.
Aidha amesema katika filamu hiyo elimu,hamasa na faida mbalimbali za huduma za DCB Commercial Banki zimeonyeshwa.
Pia amesema katika filamu hiyo imeeleza namna gani akaunti ya Wanafunzi (DCB Student Account) ilivyomsaidia kijana Jensen kupata elimu yake hata baada ya kufiwa na wazazi wake.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Consnet Group,amesema lengo hasa la filamu hiyo ni kufikisha ujumbe kwa jamii lengwa ili kupata elimu ya kutosha juu ya huduma za Kibenki.
Filamu hiyo imeandaliwa Kampuni ya Consnet Group kwa kushirikiana na Benki ya DCB yenye lengo la kuelimisha na kuhamasisha wateja,wadau na umma kwa ujumla juu ya faida za kufanya shughuli za kibenki na DCB ambazo zinabadili maisha ya mhusika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...