Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba ya ufunguzi wa Maonesho ya Muziki katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani jana ambayo hufanyika kila mwaka sambamba na utoaji wa Zawadi kwa mwaka 2015 pia kujumisha wanamuziki na wasanii mashuhuri kutoka nchi za Afrika na nchi mbali mbali Duniani.
Baadhi ya washiriki katika ufunguzi wa Maonesho ya Muziki wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutua yake jana katika viwanja vya maonesho ya muziki yanayofanyika katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani sambamba na utoaji wa zawadi kwa mwaka 2015 akiwa katika ziara ya kikazi.
Kikundi cha Matona kutoka Zanzibar kilipokuwa kikitoa burudani yake wakati wa Tamasha la Maonesho ya Muziki wa Kiafrika yanayojumisha wasanii na wanamuziki mbali mbali kutoka Afrika na Mabara mengine Duniani wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohanmed Shein alihudhuria akiwa mgeni rasmi katika ziara hiyo.
Baadhi ya Viongozi wa Ujumbe wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ziara ya kikazi Nchini Ujerumani wakiwa katika maonesho ya Tamasha la Utamaduni wa Muziki lililofanyika jana na kuiwashirikisha wasanii na wanamuziki kutoka Nchi za Afrika pamoja na mabara mengine Dunaiani katika Mji wa Wurzburg na .[Picha na Ramadhan Othman,]
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...