THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
|
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM. Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Serikali
ya Sweden inaridhishwa na kiwango cha maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania kwa
kipindi cha miaka 10 iliyopita na inadhamiria kuinua ushirikiano
baina yake na Tanzania ili kuleta maana zaidi katika maendeleo na kukua
kwa uchumi kwa ujumla.
Waziri
Mkuu wa Sweden Stefan Lofven amesema hayo jana tarehe 4, Juni, 2015 ofisini
kwake alipokutana na Rais Kikwete.
"Tumefikia kiwango kingine, tunahitaji kuanzisha awamu mpya ya
Uhusiano wetu". Waziri Mkuu Lofven amesema.
Katika
mazungumzo yao, viongozi hao wawili wamesema kuna umuhimu wa kuanzisha awamu nyingine
ya maendeleo ambayo italeta maana zaidi ambapo Rais Kikwete amesema pamoja na
ukweli kuwa uchumi wa Tanzania unakua kwa haraka, bado juhudi za kuondosha
umaskini zinahitajika na zitafanikiwa kwa kuelekeza nguvu kwenye kilimo ambacho
ndicho kinaajiri na kutegemewa na watanzania wengi zaidi hasa wanaoishi
vijijini.
"Tumefikia
awamu nyingine na ni awamu nzuri ya kudumisha uhusiano wetu, tunaweza
kushirikiana kwenye nishati, kilimo ili kukuza uchumi zaidi".
Waziri Mkuu Lofven amemuambia Rais Kikwete na Rais Kikwete akaongeza
"Pamoja
na misaada hiyo, awamu nyingine ya uhusiano baina ya Nchi mbili hizi inahitaji
pia kuona makampuni ya kutoka Sweden yanawekeza nchini Tanzania na pia kukuza
biashara baina ya nchi mbili hizi ili hatimaye Tanzania iweze kujitegemea zaidi
na kupunguza kutegemea misaada".
Mapema
kabla ya kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Rais Kikwete amekutana na Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika La Maendeleo Sweden (SIDA) Bwana Torbjorn Pettersson
ambaye amemueleza Rais kuwa; Sweden imeridhishwa na kiwango cha maendeleo na
juhudi za kupunguza umaskini nchini Tanzania, Uchumi wa Tanzania umekua kwa
wastani wa asilimia 7, katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, Pato la Taifa
limekua kutoka sola za kimarekani bilioni 14.4 hadi kufikia dola bilioni 49.2
za kimarekani, wakati Pato la Mtu kwa mwaka 2005 lilikuwa dola 375 na
mwaka 2014 limekua hadi dola 1038.
Rais
Kikwete yuko nchini Sweden kuishukuru serikali ya Sweden na Watu wake kwa
msaada wa maendeleo ambao umedumu tangu miaka ya 60. Nchi ya Sweden inaongoza kwa
kuipatia Tanzania misaada ya maendeleo na ni kutokana na misaada hiyo
Rais Kikwete ameishukuru Sweden kwa kuiwezesha Tanzania kuelekea kuwa
Nchi yenye uchumi wa Kati (Middle Income Country) na kufuzu kutoka kundi la
Nchi Masikini sana Duniani (Least Developed Country).
Rais
Kikwete pia amefanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Sweden Bwana Urban Ahlin
pamoja na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa nchini Sweden na kuwashukuru
kwa misaada ya maendeleo kwa takribani miaka 50 sasa.
Viongozi
hao wamempongeza Rais kwa kufanya ziara ya shukrani na kuwaaga kwani ni mara
chache kwa viongozi wengi wa Kiafrika kuaga na kuondoka madarakani.
Imetolewa na;
Premi
Kibanga,
Mwandishi
wa Habari wa Rais Msaidizi
Stockholm - Sweden.
5 Juni, 2015.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...