Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Technolojia, Prof. Makame Mbarawa
ameipongeza Kampuni ya HUAWEI Tanzania kwa ushirikiano wao wa karibu na
wizara katika kuchangia miradi mingi hususan mambo mengi ya TEHAMA .
Huawei
Tanzania inafanya kazi kwa ukaribu sana ni wizara na kwa hivi sasa ni
mojawapo ya Mtoa huduma za vifaa vingi vya ujenzi wa jengo jipya la DATA
center.
Data
center ni mojawapo ya ujenzi mkubwa unaofanywa na wizara ya sayansi na
jingo hili litakua na kazi ya kuhifadhi DATA za serikali pamoja na
makampuni mbalimbali ya umma na ya binafsi. Data center itakuwa
inahifadhi na kutunza kwa usalama takwimu na habari zozote kwa kutumia
sever zake na kupelekea upatikanaji wa huduma kua kwa bei nafuu na kwa
urahisi

Mkurugenzi
Mtendaji wa Huawei Tanzania Zhang Yongquan akitoa hotuba yake katika
kongamano la Huawei Cloud Conference 2015, wakitazama (kutoka kushoto
hadi kulia); Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame
Mbarawa na Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Lv Youqing.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Huawei Tanzania Zhang Yongquan na Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa wakikata utepe kuzindua rasmi
gari maalum la Huawei kwa ajili ya maonyesho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...