Mshiriki
wa Mafunzo ya utekelezaji mradi wa Kuimarisha mfumo wa
habari za hali ya hewa na mifumo ya tahadhari ya mapema nchini akichangia
wakati wa mafunzo hayo kwa wajumbe wa kamati za maafa za kata ya Makiba,
wilayani Arumeru mkoani Arusha, mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri
Mkuu kupitia mradi huo , Tarehe 13 Juni, 2015.
Mratibu
mradi kitaifa wa Kuimarisha mfumo wa habari za hali ya hewa na mifumo ya
tahadhari ya mapema nchini, Alfei Daniel akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya
utekelezaji wa mradi huo kwa wajumbe wa kamati za maafa za kata ya Makiba, Wilayani Arumeru mkoani Arusha, tarehe 13 Juni,
2015, wengine ni wawezeshaji wa mafunzo hayo.
Washiriki
kutoka kamati za maafa za kata ya Makiba, Wilayani Arumeru mkoani Arusha, wakiwa katika picha ya
pamoja na Mratibu mradi kitaifa wa Kuimarisha mfumo wa habari za hali ya hewa
na mifumo ya tahadhari ya mapema nchini, Alfei Daniel (wa kwanza kushoto) mara
baada ya kufunga mafunzo ya utekelezaji wa mradi huo, tarehe 13 Juni, 2015.
Serikali za vijiji zatakiwa kuhusisha Maafa ya mabadiliko ya
tabianchi na mipango ya maendeleo.
Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu Maafa kupitia mradi wa
kuimarisha mifumo ya habari za hali ya hewa na mifumo ya tahadhari
nchini imezitaka serikali za mitaa na vijiji nchini kuhusisha maafa
yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi na mipango yao ya maendeleo, ili
kuhakikisha jamii inakuwa na uchumi bora na uwezo wa kupunguza athari za
maafa hayo.
Akiongea wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya
Maafa wa kata ya Makiba Wilayani Arumeru, mkoani Arusha, Mratibu Mradi
huo Kitaifa, Alfei Daniel tarehe 13 Juni, 2015, alisema serikali za
vijiji zitumie taarifa za athari za mabadiliko ya tabianchi za vijiji
vyao ambazo zitakuwa zinaainishwa kupitia mradi huo kama sehemu ya
kuandaa mipango mikakati ya maendeleo vijijini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...