Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwilowe, Wilaya ya Mpwapwa, baada kuzuia msafara wake wakati alipopita katika Kijiji hicho wakati wa ziara ya kukagua Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili unaofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Kutekelezwa na Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO). Wanakijiji hao walimweleza Waziri kuwa kijiji chao pia kiunganishwe na umeme.
Wananchi wa Kijiji cha Mwilowe wakizuia msafara wa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene wakitaka kijiji hicho pia kiunganishwe na nishati hiyo. Waziri alikua katika ziara ya kutembelea na kukagua Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini unaofadhiliwa na wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kutekelezwa na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO).
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akiangalia mfano wa mashine ya kusaga inayotumia umeme wa mota aliyotengenezwa na Kijana katika Kijiji cha Lukole. Simbachawene aliahidi kumsaidia Kijana hiyo kuweza kufikia lengo lake.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akizindua Albam ya nyimbo ya Kwaya ya Mtakatifu Agustino katika Kijiji cha Kingiti, Kigango cha Kingiti, wilaya ya Mpwapwa wakati wa ziara yake ya kukagua Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini, Awamu ya Pili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...