Na
Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
SERIKALI
imeandaa rasimu ya mkakati wa mawasiliano katika sekta ndogo ya mafuta na gesi
ambayo itaweza kusaidia kutoa elimu kwa wananchi na kuwaondolea usumbufu w wa
kupata taarifa potovu kuhusu kuwepo na gesi nchini.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam leo, Katibu Tawala
wa Mkoa wa Mtwara kwa niaba ya Mkuu wa
Mkoa wa Mtwara,Fatma Dendegu,Alfred Luanda
amesema kumekuwa na uhaba wa elimu kwa wananchi juu ya masuala ya gesi
na mafuta na kusababisha vurugu katika mkoa huo.
"Wananchi
wamekuwa hawana elimu ya kutosha na kutokupewa ushirikishwaji kutoka serikalini
katika masuala ya gesi hali ambayo inapelekea wananchi kuwa na imani
potofu,"alisema.
Alisema
mkakati huo wa elimu hiyo ya mawasiliano kwa wananchi utasaidia kwa kiasi
kikubwa katika kuwahakikishia wananchi kuwa gesi iliyokuwqepo nchini ina faida
kwa kila mwananchi.
Luanda
alisema neema ya gesi iliyotokea nchini ni lazima ilindwe kwani itasaidia
katika kukuza uchumi wa nchi na kusaidia taifa kuwa katika uchumi wa kati kama
inavyotegemewa katika miaka ijayo.
"Faida
nyingine kubwa kwa kuwepo na gesi nchini ni mchango mkubwa kuzalisha gesi
hivyo itatumika kuzalisha umeme na taifa kuwa na umeme wa uhakika na
wakutosha,"alisema.
Kwa
upande wake,Meneja Mawasiliano wa Wizara ya Nishati na Madini Badra Masoud
alisema mkakati huo unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu na
baadae kuwapa wadau kuupitia na kwenda kwa wananchi.
"Mkakati
huu utakuwa ni chachu ya kuwapa wananchi kuelewa rasilimali iliyokuwepo nchini
na kuielewa faida yake na kuondokana na upotofu ambao wanaupata kutoka katika
makundi mbalimbali,"alisema.
Alisema
gesi ni raslimali ambayo ni kubwa nchini hivyo kuwepo nchini ina mchango mkubwa
hivyo ni lazima wananchi wafaidike na kuitumia rasilimali hiyo kubwa.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Fatma Salum Ally akizungumza na baadhi ya wananchi wa Wilya ya Lindi na Mtwara kuhusiana na matarajio makubwa katika sekta ya Mafuta na Gesi pamoja na uundwaji wa mikakati ya mawasiliano katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Alfred Luanda ambaye alikuwa mgeni rasmi akimwakilisha Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akizungumza katika mkutano uliokutanisha baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Lindi na Mtwara leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa wizara ya Nishati na Madaini akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Uwazi, Ushirikishwaji na uwajibikaji katika sekta ya mafuta na Gesi leo katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Mtwara na Lindi waliohudhuria katika mkutano wa kujadiliana matarajio makubwa katika sekta ya mafuta na Gesi leo jijini Dar es Salaama katika hoteli ya Serena.(Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...