Msanii Steven Mengele 'Steve Nyerere' akiwasili katika viwanja vya CCM Bwawani, kuongea na wananchi wa eneo hilo, kwa ajili ya kutangaza nia ya kugombea Ubunge wa jimbo la Kinondoni, ikiwa pamoja na kuhamasisha wananchi wajitokeze kujiandikisha. Msanii wa filamu Tanzania Steven Mengele 'Steve Nyerere' na mkewe wakisalimia na wananchi waliojitokeza katika mkutano wake wa kutangaza kuwania jimbo la Kinondoni.
Steve Nyerere akipongezwa kwa uamuzi wake wa kutangaza nia
MSANII wa filamu nchini Steven Mengere 'Steve Nyerere' (kulia) ametangaza nia ya kugombea ubunge wa jimbo la Kinondoni jijini Dar es salaam, huku akiwataka Watanzania wenzake
kujitokeza kuandikisha katika daftari la wapiga kura, ili wasikose kupiga kura katika uchaguzi mkuu
utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Akizungumza katika mkutano maalum wa kutangaza nia na kuhamasisha watu kujiandikisha, alisema
kujiandikisha ni haki ya kila Mtanzania hivyo kwa vijana na wazee hakuna sababu ya kukaa na kuacha
muda unapioga bila ya kuutumia.
Nyerere alisema ni haki kwa kila Mtanzania kwenda kujiandikisha hivyo hakuna sababu ya kuacha
kipindi hicho kinapita bila ya wao kukitumia.
"Mama zangu, Baba zangu, Vijana wenzangu, jitokezeni kujiandikisha ni haki yenu ya msingi, hasa katika uchaguzi mkuu ujao"alisema Steve Nyerere.
Pia Nyerere alisema atahakikisha anatatua changamoto za wananchi wa jimbo la Kinondoni pindi atakapopata
ridhaa ya kuliongoza jimbo hilo.
Hayo aliyasema mwishoni mwa juma wakati akitangaza nia ya kuwania ubunge wa Kinondoni kupitia Chama cha
Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Msanii huyo alisema wilaya hiyo ina changamoto nyingi ambazo zinapaswa kutatuliwa ili wananchi
waweze kuishi maisha ambayo hayana kero.
Alisema huu ni wakati wa mabadiliko na mabadiliko yataletwa na yeye kwa kuwa anazijua changamoto nyingi ambazo zinawakabili wananchi hao.
Alisema huu ni wakati wa mabadiliko na mabadiliko yataletwa na yeye kwa kuwa anazijua changamoto nyingi ambazo zinawakabili wananchi hao.
"Mimi Steve Nyerere nimeamua kwa dhati kujitoa na kutangaza nia ya kuwania ubunge ili nisaidiane
na wananchi wa Kinondoni kwa ajili ya kuijenga Kinondoni mpya," alisema Steve.
Alisema Kinondoni inapaswa kuwa ya mfano kwa kuwa na mitaa iliyopangwa katika mpangilio
maalumu na mitaro iliyosafishwa vyema.
Alisema licha ya hilo, Kinondoni inapaswa kuboreshwa miundombinu ili kuzuia mafuriko ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara na kuharibu sifa ya jimbo hilo linaloubeba mkoa wa Dar es Salaam.
Alisema licha ya hilo, Kinondoni inapaswa kuboreshwa miundombinu ili kuzuia mafuriko ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara na kuharibu sifa ya jimbo hilo linaloubeba mkoa wa Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...