MKUU wa Wilaya (DC) mstaafu,
Margaret Kipaya (75) (pichani) amefariki dunia kutokana na matatizo ya kisukari baada ya
kuugua kwa miezi kadhaa.
Taarifa ya familia ya DC huyo
ilisema Margaret alifariki dunia alfajiri ya kuamkia jana katika Hospitali ya
Emilio Mzena jijini Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa kesho nyumbani kwake
Makongo Juu.
“Marehemu atazikwa keshokutwa
(kesho) kwenye makaburi ya Makongo baada ya makubaliano ya familia
kufikiwa,”ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Miaka ya mwisho ya utumishi
wake, Margaret ambaye anatokea Kahama mkoani Shinyanga, alifanya kazi kama Mkuu
wa wilaya za Nzega na Igunga mkoani Tabora kwa nyakati tofauti na Songea mkoani
Ruvuma hadi alipostaafu.
Alianzi utumishi wakekwa kufanya
kazi kwa mtindo wa kujitolea akiwa Katibu wa UWT Wilaya ya Mzizima, Dar es
Salaam mwaka 1967.
Mwaka 1968, alichaguliwa kufanya
kazi ya kumhudumia mke wa hayati Patrice Lumumba akiwa Ikulu, Dar es Salaam na
baadaye mwaka huo huo alijiunga na kozi ya miezi tisa katika Chuo cha Siasa
Kivukoni.
Mwaka 1969 alirudi UWT Mzizima,
lakini safari hii akiwa Katibu wa Wilaya kwa kuajiriwa na mwaka uliofuta
alichukuliwa na Makao Makuu ya Umoja wa Vijana Tanzania (UVT) kwa ajili ya
mafunzo ya halaiki yaliyokuwa yakitolewa na Wakorea.
Baada ya mafunzo hayo,
aliteuliwa kuzunguka nchi nzima kwa ajili ya kutathmini maendeleo yaliyopatikana
baada ya miaka 10 ya Uhuru kwa ajili ya kuwaonyesha Waingereza waliokuwa
wamealikwa kwenye sherehe za Uhuru za mwaka 1971. Pia, alikuwa msimamizi wa
halaiki.
Mwaka uliofuata aliteuliwa
kwenda Zanzibar kuongoza walimu 10 kufundisha vijana halaiki kwa ajili ya
tamasha la Vijana wa Afrika lililofanyika Zanzibar mwaka 1973.
Pia, mwaka huo huo aliteuliwa
kuandaa tamasha la sherehe za miaka 20 ya TANU zilizofanyika mwaka uliofuata
jijini Dar es Salaam.
Marehemu ameacha watoto watatu,
wajukuu 14 na vilembwe wanne.
R.I.P mama Margaret.
ReplyDeleteKama kuna Vilembwe bila shaka kuna Vitukuu