Taasisi ya John Mashaka Foundation pamoja na American Engineering Group (AEG) hatimaye imeweza kuwasaidia wanakijiji 3,500 katika kijiji cha Manila wilayani Rorya kupata maji safi na Salama. Mradi huu umegharimu kiasi cha Shilling Billioni moja. Kabla ya huu mradi, wananchi wa hiki kijiji walikuwa wakitembea kilometa 24 kwenda ziwani na kurudi. Kazi ambayo ilikuwa ikifanywa na watoto pamoja na Wanawake.

Huu ni mradi wa aina yake, kwani unatoa maji safi na salama. Na ina uwezo wa kusafisha kiasi cha lita 100,000 kwa siku ambayo inakuwa safi na salama kwa kiwancho cha 99.9%. Mitambo hii imeagizwa moja kwa moja kutoka Marekani, ambako ilibuniwa katika chuo kikuu cha Massachussets Institute of Technology, kwani haihudumiwa kwa namna yoyote ile ile. Inajitegemea na kujiendesha kwa kutumia nishati ya jua. Pampu ya maji ina uwezo wa kufanya kazi kwa miaka 20.
Mafundi Wakichota maji kwenye kisima cha Zamani, ambayo ilikuwa ni ya Msimu.
Mafundi Wakishauriana Jambo. Huu mtambo ni wa aina yake. Unatumia solar na inaweza kupandisha maji kiasi cha lita 20,000 kwa saa. Na inachuja maji kwa ubora wa 99.9% ambayo ni safi na salama.
Mkuu wa mkoa wa Mara, Col. (Rtd) Aseri Msangi akiongea na wanakijiji kuhusu manufaa ya huu mradi wa maji kwenye maisha yao.
Wakina Mama watakaosimamia mradi wa maji wakipiga picha ya Pamoja mbele ya Matenki ya Maji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 22, 2015

    Hii ni kazi nzuri, jua tunalo tulitumie, ila mshirikishe wenyeji walionufaika na mradi huu na halmashauri husika ili kazi ya kurekebisha mabomba na kuhakikisha usafi wa maji kwa kiwango kinachotakiwa uwe endelevu, isije bomba likaharibika wenyeji wasijue la kufanya. Tuangalie pia kuwezesha sehemu nyingine zenye shida kama hii kwa kutumia ujuzi huu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 22, 2015

    John Mashaka tumekumiss sana kiongozi. Ubunge lini bwana. Bunge la 2015 inahitaji vijana makini, na hii ni kampeni tosha kule Rorya.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 22, 2015

    huyu bwana Mashaka John, amejaliwa kitu kioja. Ana Akili. Tanzania ingekuwa na vijana 10 kama huyu tungefika mbali sana. Ni vijana wachache sana kama Mashaka mbao wanajitolea kusaidia jamii. Wengi wanarudi hapa mjini na kutuleta vuturugu na hela zao za sembe. Kazi nzuri sana bwana Mashaka. Kweli wewe ni mfano wa kuigwa.
    Usiishie hapa. endelea na uvifikie vijiji vingine ambavyo havina maji, kwani Mungu kakupa nafasi uliyonayo ili kuisaidia jamii. Mungu akuongezee maradufu

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 22, 2015

    Endelea na moyo huo huo kijana. Hii inapendeza sasa hao wakina mama wakafanye shuguli za maendelo

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 22, 2015

    Ankal,
    hahutendei haki wasomaji wa blog ya jamii. huyu kaka , john mashaka ni wadau wakubwa ambao walikuwa wanachangamsha hii blogu haijawahi kutokea. tunaomba arudi ulingoni. tunamuomba ndugu yetu mashaka atuletee hoja zake murua za kutuelemisha umma wa kitanzania.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 22, 2015

    Safi sana mkuu John Mashaka kwako wewe mimi sina shaka hata kidogo, tunataka maendeleo lkn pia tunataka nakala zako za kuelimisha ziendelee kutoka kama pale mwanzo

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 22, 2015

    Huu ndio uzalendo wa kweli. Nimeguswa sana na moyo wa huyu kaka. Bahati mbaya nishaolewa, ningeshatuma maombi. Mungu akubariki

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 22, 2015

    ankal we noma sana. unajua huyu jama ukimuweka mbele kila mtu atataka kusoma hii blogu. kwa historia fupi, john mashaka ndio mmoja wa wa magwiji wa kiuchumi. amekuwa akitoa mihadhara mingi sana kwenye hii blogu, na amejenga wafuasiw engi sana kiasi wkamba anaitwa nabii yohana. Kwa kabila ni mkurya wa tarime, ila ni kichwa balaa. ongera sana john kwa kazi unayowafanyia watu wako wa musoma

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 23, 2015

    Asante sana Kaka Michuzi kwa habari nnjema, nzuri. John Mashaka hongera sana kwa kufanikiwa kuanza mradi huo. Kwa kweli ninafahamu kuna wengi wapo ukingoni wanatamani sana kufanya mazuri ila swala la vikwazo vidogo vidogo vina katisha tamaa.
    Pengine kukiwa na habari za mara kwa mara kuhusu wawekezaji, basi watu watakuwa ma moyo wa kuisaidia jammii yetu huku.
    Wapo wengi wanasaidia sana jamaa zao huku, ila ndugu au marafiki hawasemi.
    Asante Kaka Michuzi na hongera sana John Mashaka.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 23, 2015

    tulikuwa na amani kwa m,uda mrefu kwenye hii blog. john Mashaka ameletwa, wabeba boxi watakuja humu kuanza kutoa hasira zao na matusi ya kufa mtu. ukitaka kujua wanaokaa majuu wana hasira zao, mweke huyu jamaa utakiona cha moto. Haisee, kazi kweli kweli, nawapisha wenye nguvu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...