Twaha Sultan akionyesha mpira anaotumia kwa ajili ya kujisaidia hali ambayo inampa maumivu makali pamoja na kupata gharama kubwa ya kubadilisha mpira kila baada ya wiki tatu.
Mama mdogo wa Sultan, Sarha akionyesha uvimbe unaomsumbua mtoto Twaha sultan.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sitti Tanzania Foundation, Sitti Mtemvu akizungumza baada ya kukabidhi msaada wa shs laki mbili kwa ajili ya kusaidia matibabu yake.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sitti Tanzania Foundation, Sitti Mtemvu (kushoto), akimkabidhi msaada wa sh. laki mbili, Sarha Magamba, jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kusaidia matibabu ya mtoto, Twaha Sultan (17), mkazi wa Kipawa Karakata (katikati), ambaye ana uvimbe wa kilo nne na nusu mgongoni.Yeyote atakayeguswa na tatizo la mtoto huyo anaweza kuwasiliana na mlezi wake kupitia namba ya simu 0713970491.
daah jamani mbwembwe zote hizi kumbe msaada wenyewe laki 2!!? well it is something lakini Siti walau ungeorganize rafiki zako na ndugu nk ili walau mtoe kitu significant....else ungeenda kimya kimya bana...hongera lakini
ReplyDeleteMwache, amejitolea kajitahidi wewe ukitaka kutoa si uombe simu nawe uchangie
ReplyDelete