Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro
Premium Lager, leo imepoteza mchezo wake wa kwanza kuwania kufuzu kwa
fainali za AFCON mwaka 2017 baada ya kufungwa kwa mabao 3 - 0 na wenyeji
Misri.
Taifa
Stars ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na hasa sehemu ya ulinzi
ilifanya kazi ya ziada kuokoa mashambulizi ya washambuliaji wa timu ya
Misri, na kupelekea kwenda mapumziko -0 - 0.
Kipindi
cha pili Misri walifanya mabadiliko yaliyowapelekea kupata mabao hayo 3
ndani ya dakika 10, kupitia kwa Ramy Rabia(60), Basem Morsy(64) na
Mohamed Salah (69).
Stars
ilifanya mabadiliko ya kuwaingiza Frank Domayo, Saimon Msuva na Salim
Mbdonde na kufanya shambulizi kadhaa langoni kwa Misri lakini
mashambulzi hayo yaliokolewa na walinzi wa timu ya Misri.
Mara
baada ya mchezo huo, Taifa Stars inaondoka leo Alexandria kuelekea
Cairo ambapo itaondoka na shirika la ndege la Ethiopia saa 8 usiku na
kufika jijini Dar es salaam jumanne saa 7 mchana.
Tanzania:
Deogratias Munish, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Aggrey Morris/Salim
Mbonde, Nadir Haroub, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto/Saimon
Msuva, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samata, Amri Kiemba/Frank Domayo.
Misri:
Ahmed El Shenawy, Ahmed Hegazy, Ramy Rabea, Mohamed Abd Elshafy, Hazem
Emam, Mohamed Elneny, Ibrahim Salah, Mahmoud Abd Elmonem/Ramadan Soffiy,
Mohamed Salah/Mostafa Ftahy, Doly Elgabay/Basem Morsy, Ahmed Hassan
Meky.
USAJILI WA WACHEZAJI KUANZA JUNI 15
Kikosi cha timu ya Taifa Taifa stars.
kWANI LAZIMA SISI TANZANIA KUSHIRIKI HAYA MASHINDANO AU KUCHEZA SOKA TUJARIBU BAO LABDA TUNAWEZA KUFIKA MBALI HII KUTUPA FEDHA NA KULITIA AIBU TAIFA LAZIMA TUCHOKE SASA IKO HAJA YA KUJITOA KATIKA MASHINDANO YA KIMATAIFA KWA MIAKA MITANO HUKU TUKITAFUTA VIPAJI KUANZIA MIAKA 17 VIJANA WAPYA WOTE SIO HII KAZI YA KU "RECYCLE" KILA MWAKA NA MATOKEO NI YALE YALE TUFIKIRI NJE YA SANDUKU AU ILE TAFSIRI YA MWENDA WAZIMU NDIO SISI,KUFANYA KITU KILE KILE NA KUTARAJIA MATOKEO TOFAUTI.
ReplyDeleteMDAU.
ALEXANDRIA,MISRI.
Niliangalia mechi hii.Taifa stars ni kichekesho ilicheza kibaya ni kama umewakusanya wachezaji kutoka mtaani masaa mawili kabla ya mechi. Hawana mpangilio na wangefungwa hata bao kumi kama WaMisri wangekuwa makini. Asilimia kubwa walikuwa wamisri waliotawala mechi. Hii ni aibu na Tanzania ifikirie kujitoa kwenye hii michezo na wajenge timu kwanza.
ReplyDeleteMdau Sweden.