Mgeni Rasmi katika Semina ya Kukuza Uelewa wa Usimamizi wa Mazingira kwa Watendaji wa Halmashari ya Jiji la Tanga, Bwana Salim Chima ambaye pia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga akifungua Semina hiyo ya siku moja iliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Julius Ningu akizungumza jambo katika Semina ya Kukuza Uelewa katika Masuala ya Mazingira kwa Watendaji wa Halmashari ya Jiji la Tanga iliyofanyika jijini humo leo.
Sehemu ya Washiriki wa semina ya siku moja ya Kukuza Uelewa katika Masuala ya Mazingira kwa Watendaji wa Halmashari ya Jiji la Tanga wakisikiliza mada zinazotolewa katika warsha hiyo
Mgeni Rasmi katika Semina hiyo Bwana Salim Chima akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wote walioshiriki katika Seminas hiyo. 

 Na Victor Mariki - Ofisi ya Makamu wa Rais

Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira imebainisha kuwa takribani ya asilimia 61 hadi 75 ya eneo la ardhi ya Tanzania imeathirika na janga la ukame ambao unaweza kupelekea uzorotaji katika ukuaji  wa uchumi  na hata kutoweka kwa baadhi ya viumbe hai.

Hayo yalielezwa  na Afisa Mazingira wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi Zainab Shaban Bungwa wakati akitoa mada katika  semina ya kukuza uelewa wa masuala ya usimamizi wa mazingira  kwa watendaji wa Halmashauri ya jiji la Tanga mkoani humo leo.

Aidha Bi Bungwa alifafanua kuwa  uchumi wa Tanzania  unategemea kwa kiasi kikubwa  rasimali asili kama vile ardhi, misitu, wanyamapori na maji ambapo inakadiriwa  asilimia 75 ya wanachi waishio vijijini hutegemea zaidi ardhi katika uendeshaji wa maisha yao.

Pia aliongeza kuwa  Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira imechukua hatua mbali mbali katika kukabiliana na  janaga hilo  kwa kuunda sera, mikakati na sheria mbalimbali  za kudhibiti uharibifu wa mazingira nchini.

Baadhi ya mikakati, sera na sheria hizo  ni Mkakati wa Hatua za Haraka Kuhifadhi Mazingira na Vyanzo vya Maji, Mkakati wa Bahari na Mabwawa, Program za Kupambana kwa Kuenea Hali ya Jangwa na Ukame, Mkakati wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi pamoja na Program na Miradi inayotekelezwa na  Sekretarieti ya Mikoa katika suala la Utunzaji Mazingira.

Sanjari na hayo Bi Bungwa alienda mbele zaidi  kusema kuwa hivi sasa robo ya dunia ipo hatarini kukumbwa na hali ya jangwa kwa kuwa  zaidi ya hekta bilioni 3.6 za ardhi yake tayari zimeshaathiriwa na janga hilo ambalo mpaka sasa limeathiri zaidi  ya watu milioni 900  duniani kote .

Kwa upande wa bara la Afrika  hivi sasa hali hiyo ya jangwa imekuwa ni tatizo sugu  kwakuwa mpaka sasa tayari asilimia 73 ya ardhi yake  imeshathirika vibaya na janga hilo hali ya jangwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...