Halmashauri 13 za Mikoa ya Njombe na Arusha zinaanza kunufaika na miradi ya kupunguza Umaskini ya OPEC Awamu ya tatu kwa Watu takribani Milioni 3.1 utakaotekelezwa kwa Miaka Mitatu kati ya January 2015 na Desemba 2017.
Hayo yameelezwa mapema leo hii na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, IKULU bwana Peter Ilomo wakati akizindua kikao kazi cha kuanza kwa Viongozi na Watendaji wa Mkoa Njombe juu ya utekelezaji wa miradi hiyo ya kupunguza umaskini kwa ufadhili wa OPEC awamu ya tatu. Bw. Ilomo amesema kuwa Lengo la utekelzaji wa miradi hiyo ni Kuboresha upatikanaji wa huduma za kiuchumi na Kijamii kwa Kaya Maskini zilizotambuliwa na kuandikishwa katika Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Halmashauri huzo.
Aidha Bwana Ilomo amesema kuwa katika mradi huo jamii zitatekeleza miradi ya elimu, afya na maji pale patakapoonekana pana upungufu wa huduma hizo . Nae Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF amezitaja Halmashauri zitakazohusika kwa katika Mikoa hiyo kuwa ni Ludewa, Makete, Njombe, Wanging'ombe na Halmahshauri za Mji Makambako na Njombe ambazo zote ni za Mkoa wa Njombe na akazitaja za Mkoa wa Arusha kuwa ni Longido, Monduli, Ngorongoro, Arusha, Meru, Karatu na Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Pamoja na miradi ya kupunguza umaskini ya OPEC, TASAF pia inatekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika halmashauri zote nchini ikiwa ni pamoja na Unguja na Pemba na tayari. Zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali katika kukao hicho.
Mkurugenzi mtendaji wa TASAF akitoa maelezo ya utangulizi juu ya miradi ya kupunguza umasikini ya OPEC awamu ya tatu.
Katibu mkuu ofisi ya Rais Ikulu Peter Ilomo akizindua mkutano wa kazi juu ya utekelezaji wa miradi ya kupunguza umasikini ya OPEC awamu ya tatu Mjini Njombe leo.
Kaimu mkuu wa Mkoa wa Njombe ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba akielezea hali halisi ya utekelezaji wa shughuli za TASAF katika mkoa wa Njombe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...