kikosi cha baobab
Mchezaji wa timu ya soka wa waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa fc), Martin Peter (Jezi ya kijani kulia) akipambana na mmoja wa wachezaji wa Timu ya Makipa, Ivo Mapunda.

Na Mwandishi wetu
TIMU ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa FC) Ijumaa hii itacheza mchezo maalum wa kirafiki dhidi ya timu ya wafanyakazi wa shule ya sekondari ya Baobab ya Bagamoyo.

Mchezo huo umepangwa kuanza saa 10.00 jioni kwenye uwanja wa Shule ya sekondari ya Baobab na mgeni rasmi atakuwa Mkurgugenzi wa Shule hiyo, Hlafan Swai.
Mbali ya Swai, viongozi wengine wa shule hiyo watahudhuria mechi hiyo maalum kwa ajili ya kuhamasisha michezo shuleni hapo.

Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary amesema kuwa awali walipanga kucheza mechi mbili, ya wanaume (mpira wa miguu) na wanawake (netiboli), hata hivyo wachezaji wa Taswa Queens hawakuweza kuanza mazoezi na hivyo kulazimika kufuta mechi hiyo.

Majuto alisema kuwa wamepokea maombi kutoka uongozi wa shule hiyo na hasa baada ya kutoa mwanafunzi bora kitaifa katika mtihani wa kidato cha nne, Nyakaho Marungu. 

Alisema kuwa wamehamasika kupata mwaliko huo ambapo mechi hiyo itakuwa kama sehemu ya sherehe ya kufunga shule.

Baadhi ya wachezaji wa Taswa FC wakataokuwepo katika mechi hiyo ni Ali Mkogwe, Wilbert Molandi, Salum Jaba, Deogratius “Super Deo” Maganga, Julius Kihampa, Sweetbert Lukonge, Elius Kambili, Zahoro Mlanzi, Frank Balile, Mwarami Seif, Saidi Seif, Jose, Martin Peter, Athuman Jabir, Muhidi Sufiani na  Jabir Johnson.

Baadhi ya wachezaji wa  timu ya wafanyakazi wa shule hiyo ni John Kanakamfumu, Herry Morris (kocha wa timu ya wanafunzi), Renatus Kavishe, David Ntungi, Hadji Juma, Madata Lubigisa, Athuman Tippo na wengineo.

“Huu ni mchezo wa kudumisha ushirikiano wetu kwani sisi ni waandishi wa habari za michezo na pia ni wazazi, hivyo tunaweza kuwapeleka watoto wetu kusoma kaika shule hiyo bora, hivyo nawaomba wachezaji wote wafike kwa wingi ili kuona mechi hiyo ya aina yake,” alisema Majuto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...