Picha na
maktaba
Na Woinde
Shizza,Arusha
Mamlaka
ya Chakula na dawa(TFDA) na Shirika la Viwango nchini(TBS), wameshauriwa
kuwadhibiti zaidi wafanyabiashara wasio waaminini ambao wanaingia nchini bidhaa
sizizo na ubora kwani wanaporomosha uchumi.
Meneja
masoko wa kampuni ya Wrigleys (EA)
Company Ltd, Emanuel Laswai, alitoa kauli hiyo juzi, katika uzinduzi wa bidhaa
mpya za kampuni hiyo ya Doublemint
nchini Tanzania.
Laswai
alisema, uingizwaji wa bidhaa feki na zisizo na ubora zina
athari za kiuchumi na kiafya kwa watumiaji wa
bidhaa hizo.
“sisi
kampuni yetu kwa mwaka tunalipa kodi Tsh 120 milioni, lakini inaumiza kuona
kuna bidhaa zinaingizwa nchini kinyamela bila kulipiwa
kodi”alisema
Alisema
bidhaa zao zote kabla ya kuingia sokono lazima ziidhinishwe na vyombo vya
ukaguzi wa serikali kama TBS na TFDA.
Mkaguzi
wa vyakula, dawa, vipodozi ,wa mamlaka ya chakula na dawa TFDA,kanda ya
kaskazini, Barnabas Jacob, akizungumzia tatizo la uingizwaji bidhaa feki
alisema Mamlaka hiyo, imeendelea kudhibiti na kukamata na kutekeleza bidhaa
hizo.
Jakob
alisema milango ya TFDA, iko
wazi kwa kila mwananchi
kutoa taarifa ya kuwepo kwa bidhaa hatarishi katika mazingira yeyote ili ziweze
kuchukuliwa hatua za kudhibiti bidhaa
zisizofaa kwa matumizi ya binadamu.
Kwa
Upande wake, Afisa uhusiano wa shirika
la viwango nchini(TBS) Roida Andusamile akizungumza na Mwananchi alisema TBS
itaendelea kudhibiti bidhaa zisizo na ubora kuingia
nchini kwa kuanza kudhibiti bidhaa hizo
kutoka nchi
zinapotoka.
Hata
hivyo, alisema ni wajibu wa wananchi pia kutoa taarifa TBS wanapobaini bidhaa
zisizo na ubora katika soko au ambazo bado hazijaidhinishwa na vyombo vya
serikali, ili kuweza kuchukuliwa hatua mara moja ya kuwadhibiti na kuwakamata
wahusika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...