Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii, Tabora.
Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta amesema kuwa anataka Urais wa miaka mitano kuweza kuivusha nchi katika kutokana na mambo yanayoonekana ikiwamo muungano,udini ,ungezeko la vijana.
Sitta ameyasema hayo leo wakati akitangaza nia ya kugombea urais katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chifu Fundikira Kata ya Itetemia mkoani Tabora.
Amesema mtu yeyote makini ana nafasi ya Urais, hana budi kuyapima mazingira ya taifa katika miaka mitano ijayo na kuzielewa changamoto zitakazokuwepo katika kipindi cha uongozi anachokusudia kuongoza.
“Maoni yangu kipindi cha miaka mitano ijayo kina mwelekeo wa mifarakano katika masuala ya muungano wetu; kutetereka kwa mshikamano wetu kunatokana na chokochoko za siasa za ushindani, udini na kupanuka kwa tofauti ya kipato, ongezeko la kundi kubwa hususani la vijana mijini lisilo na uhakika wa ajira na haya yote yanaashiria ongezeko la uhalifu”amesema Sitta.
Amesema anamini kutokana na mchanganyiko wa uzoefu wa uongozi, unamuwezesha kukusanya nguvu chanya za Watanzania ili kuyatanzua matatizo yanayotokana na changamoto zilizopo kwa kipindi cha sasa.
Sitta amesEma kugombea nafasi ya Urais wa nchi yetu si jambo jepesi.Linahitaji tafakuri ya kina ukizingatia kuwa nafasi hiyo ya uongozi inabeba matumaini ya watanzania wote milioni 47.
Amesema Ili kukuza uchumi wa nchi kwa kasi inayopunguza umaskini kwa haraka na huku tukijenga uwezo mkubwa zaidi wa bajeti ya serikali kutosheleza ubora wa huduma za jamii kama vile afya, elimu na maji, hatuna budi kufanya jitihada za makusudi za kuubadili mfumo wa uendeshaji nchi uwe ni wa motisha kwa wazalishamali.
Mifumo ya nchi zilizopiga hatua kubwa za maendeleo duniani ni ile iliyoweka mazingira chanya ya kuaminiana baina ya serikali na sekta binafsi. Hali hii haijatimia hapa kwetu.
Aidha Wafanyabiashara wakubwa wa ndani hawawekezi vya kutosha ndani ya nchi kuleta maendeleo ya haraka ya huduma, viwanda,kilimo na biashara. Baadhi yao, kwa hakika baada ya kuchuma fedha wanazihamishia nje ya nchi. Matokeo yake ni kwamba uchumi haukui kufikia kiwango cha kutosheleza vipato vya wakulima na wafanyakazi na wafanya biashara.Hatuna budi kujenga muafaka na wafanyabiashara hususani wazawa wa nchi yetu. Kazi hii ina hatua mbili:
Amesema wafanyabiashara watachukuliwa hatua kwa wasio waaminifu kwa kukwepa kodi, wanaotorosha fedha za kigeni na wanaoshiriki katika rushwa kubwa na biashara za magendo,kuwepo kwa mshikamano baina ya wafanyabiashara waovu na watendaji serikali kunachochea rushwa na kudumaza uchumi. Hali hii lazima irekebishwe.
Mheshimiwa
Sitta akisimikwa kuwa Mjukuu Mkuu wa ukoo wa Fundikira katika hafla
iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu ya Unyanyembe Itetemia mkoani
Tabora jana.
Mheshimiwa
Samweli Sitta akiwa na viongozi wenzake wa CCM alipokuwa akitangaza nia
ya Kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa
Samweli Sitta akitangaza nia mbele ya umati wa wananchi katika uwanja
wa Ikulu ya Unyanyembe katika manispaa ya Tabora.
Miaka 5 - Uliza Nkurunzinza. Wenzio walikwishastaafu zamani sana wewe bado upoupo tu. Sasa unasema miaka 5 tu. Si uongo tu huo?
ReplyDeleteMiaka mitano wewe sasa upate...wewe ni kiongozi hodari, unaheshimiwa, umefanya kazi safi miaka mingi, bila corruption yoyote. Kura yangu ishapata....
ReplyDelete