THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, STATE HOUSE, 1 BARACK OBAMA ROAD, 11400 DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
mpya ajaye nchini Tanzania anakabiliwa na changamoto kubwa ya kuhakikisha
Tanzania itaendelea kubakia kuwa moja kwa kudumisha Umoja wetu na Amani kwani
Tanzania inatokana na muungano wa nchi mbili.
Rais
Jakaya Kikwete ameyasema hayo jijini Stockholm - Sweden ambapo alikuwa akiongea
na watanzania waishio Sweden mara baada ya kuwasili na kuanza ziara ya kikazi
ya siku 3, kuanzia tarehe 3 - 5 Juni,2015.
"Hapa
tulipofikia lazima kuhakikisha Taifa linakuwa moja, kuna vyama, na makabila mbalimbali, lazima uhakikishe Nchi
inabaki moja". Rais amesisitiza.
Watanzania
mbalimbali walioko nchini Sweden kwa ajili ya shughuli za kikazi, kimasomo na
ambao wanaishi nchini Sweden, walifika kumpokea na kumsalimia Rais Kikwete
ambapo pia wamemsomea risala ambayo pamoja na vitu vingine wametaka kujua
kuhusu haki yao ya kupiga kura katika uchaguzi Mkuu ujao.
"Swala
hili linategemea Tume ya Uchaguzi, likiwekewa utaratibu linawezekana. Taratibu
zake hazijawekwa, lakini ninaamini kuwa uchaguzi ujao unakuwa uchaguzi wa
mwisho ambao watanzania wanaoishi nje hawapigi kura".
Rais amesema.
Rais
Kikwete pia ameelezea matumaini yake kuwa Tanzania itapata kiongozi mzuri na
kuelezea mafanikio ambayo serikali yake imeyapata na kutumaini kuwa
yatadumishwa na kuendelezwa na Rais ajaye.
Mapema
akisoma risala ya watanzania, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Nchini Sweden
Bw. Tengo Kilumanga, amempongeza Rais Kikwete kwa kuridhia na kuonesha nia ya
dhati ya kumaliza kipindi cha uongozi wake na kuwa mfano bora katika ukanda wa
Afrika Mashariki.
"Tunakupongeza
mheshimiwa Rais, viongozi wengi katika Bara la Afrika huwa hawaagi, umefanya
kitendo cha kishujaa sana. Viongozi wa Afrika huwa hawaagi kwa sababu siku ya
kuondoka madarakani huwa haijulikani".
Amesema Bwana Kilumanga. "Hii inaonesha wewe sio Mtu wa kupenda
madaraka". Ameongeza.
Hii
ni ziara ya kwanza ya Rais Kikwete ya kuaga Nchi wahisani na wenza katika
maendeleo na Rais ameanzia Nchi za Nordic kwa sababu ya historia na uhusiano wa
Nchi hizi kwa Tanzania tangu kupata Uhuru wake.
Rais
Kikwete anaendelea na ziara yake nchini Sweden ambapo anatarajia kufanya
mazungumzo na wafanyabiashara na wawekezaji mbalimbali kwa lengo la
kuwahamasisha kuja kuwekeza nchini Tanzania.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Stockholm - Sweden
5 Juni, 2015.
Rais ajaye aunganishe watanzania na kuwa na uwezo wa kuongoza nchi. Tanzania inastahili kiongozi bora na mahiri.
ReplyDelete