Watu wenye silaha wameshambulia hoteli moja ya kitalii iliyoko kwenye pwani ya Tunisia na kuwauwa watu 37.
Maafisa wa serikali ya Tunisia wamesema kuwa mmoja wa washambuliaji hao aliuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa ulinzi na kuwa waliosalia bado wanasakwa na polisi.
Shambulio hilo lilitokea katika mji wa Sousse, ambao huwavutia maelfu ya watalii kutoka bara Ulaya na Afrika ya Kaskazini.
Hili lilikuwa shambulizi la pili dhidi ya hoteli ya watalii nchini Tunisia katika kipindi cha miezi michache iliyopita.
Inaaminika kuwa washambuliaji hao waliwavamia watalii ufukweni.
Mnamo mwezi Machi mwaka huu, wanamgambo wa Kiislamu waliokuwa wamejihami kwa bunduki waliwauawa zaidi ya watu 26 katika makavazi ya Bardo, iliyoko katika mji mkuu wa nchi hiyo Tunis.Makavazi hayo ya Bardo hilo lilikuwa maarufu sana kwa watalii.
October mwaka wa 2013, mlipuaji wa kujitoa, alijilipua nje ya nyumba moja mjini Sousse, baada ya maafisa wa polisi kutibua jaribio lake la kutaka kuingia ndani na kuishambulia.
Chanzo BBC Swahili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...