Bendi ya African Stars maarufu kama Twanga Pepeta Ijumaa Juni 12 itafanya onyesho maalum la kumtambulisha mwanamuziki maarufu nchini Ali Choki na wengine waliorejea kwenye bendi hiyo.
Onyesho hilo litafanyika usiku katika ukumbi wa Da West Park, Tabata.
Mratibu wa onyesho hilo Joseph Kapinga wa Keen Arts na Bob Entertainment amesema kuwa onyesho hilo pia litakuwa ni la vunja jungu kabla ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kapinga alisema pia Choki atatumia onyesho hilo kutambulisha nyimbo zake mpya ambazo ni “Kichwa Chini” na “No Discussion”.
Wanamuziki wengine ambao watatambulishwa pamoja na Choki ni mnenguaji wa bendi hiyo Super Nyamwela na mpiga kinanda Victor Mkambi. Choki na Nyamwela wametokea kwenye bendi ya Extra Bongo wakati Victor Mkamba ametokea bendi ya Ruvu Stars.
Kwa upande wake Ali Choki alisema kwenye onyesho hilo litakuwa ya aina yake kwani atapiga nyimbo zote alizizowahi kupiga akiwa na Twanga Pepeta kabla hajahamia bendi ya Extra Bongo.
Baadhi ya nyimbo hizo ni “Kisa Cha Mpemba,” “Fainali Uzeeni,” “Umbea Hauna Posho,” “Jirani,” “Password,” “Kuolewa,” “Busu la 2005,” “Busu la Kufunga Mwaka,” “Aminata” na zinginezo.
Naye Mkurugenzi wa bendi hiyo Asha Baraka amesema onyesho ya leo litakuwa ni kama zawadi kwa wakazi wa Tabata na vitongoji vyake, kwani itakuwa onyesho la mwisho la bendi hiyo kabla mfungo wa Ramadhani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...