WAANDAAJI wa Tamasha la Pasaka wamesema kuwa DVD ya onesho la Miaka 15 ya tamasha hilo lililofanyika Aprili mwaka huu ipo mtaani.
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema jana kuwa DVD imeonesha shughuli nzima ya tamasha hilo lililofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na mgeni rasmi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
 
“Nawaomba mashabiki wa muziki wa Injili ambao walikuwa wakiniulizia kuhusiana na DVD hiyo kwamba sasa ipo mtaani na ni jukumu lao kuitafuta katika maduka yetu.
 
“Wale waliohudhuria tamasha hilo na wale ambao hawakuhudhuria wote watambue kuwa sasa wanaweza kuona tamasha hilo wakiwa sebuleni kwao,” alisema Msama.
 
Alisema tamasha la mwaka huu lilikuwa tofauti na matamasha mengine yaliyopita kwani liliendana na sherehe za miaka 15 tangu waanze tamasha hilo.
 
Alisema DVD hiyo inaonesha waimbaji wote mahiri waliohudhuria na kwamba ana matumaini makubwa mashabiki watakuwa na kumbukumbu kubwa ya shughuli hiyo.Waimbaji mbalimbali wa ndani na nje walishiriki tamasha la mwaka huu akiwemo Mwingereza, Ayobami David na Rebecca Maloppe wa Afrika Kusini.
 
Mwaka huu Tamasha la Pasaka lilitimiza miaka 15 tangu kuasisiwa kwake na Kampuni ya Msama Promotions ya Dar es Salaam, ambapo limekuwa likijiongezea umaarufu na kukubalika zaidi kutokana na ubunifu wake wa kufanya maadhimisho ya Sikukuu za Pasaka na Krismasi kwa umahiri na mguso wa kiroho kupitia matamasha hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...