Hivi
ndivyo hali ilivyo katika barabara hii ya Viwandani, Chang'ombe jijini
Dar es salaam. uharibufu huu wa barabara umetokana na Mvua kubwa
zilizokuwa zikinyesha maeneo mengi hapa nchi majuma kadhaa yaliyopita.
Cha ajabu katika eneo hili bado maji ni mengi sana yametuama na huku
uharibifu mkubwa wa barabara ukiendelea. Mzee wa Mtaa kwa Mtaa
alibahatika kuzungumza na wadau kadhaa waliopo jirani na eneo hilo,
ambapo walisema kuwa kuja kwa Dimbwi hilo ni kutokana na kutokuwepo kwa
sehemu ya kusafirishia maji hayo kutokana na ujenzi holela wa Maghala na
Viwanda vilivyolizunguka eneo hilo, hali inayopelekea kuwepo kwa adha
hiyo kwa sasa. Je ni kweli kwamba ujenzi holela katika maeneo haya unapelekea kujaa kwa maji haya barabara??? Wataalam wa barabara tunaomba majibu. Picha zote na Othman Michuzi.
Ile
kauli ya "Kufa kufaana" ndiyo inayotumiaka hivi sasa katika eneo hili,
kwani kuna baadhi ya vijana ambao wanaombea maji haya yaendelee kuwepo
ili na wao wajipatie chochote kitu ili siku zisonge mbele. Pichani ni
mmoja wa vijana hao akiiongoza moja ya gari kupita katika eneo salama
bila kukwama, ambapo ujira wake ni kuanzia shilingi Elfu moja na
kuendelea kutegemena na ubinaadamu wako.


Du umasikini usieolezeka. Kwa shilingi elfu moja anachukua risk na kupita kwenye hayo maji machafu yaliyotuama na kuweza kuambukizwa magonjwa. Ndio maisha bora kwa kila Mtanzania. Rais Kikwete anakuja huku nchi za Scandinavia na kuwadanganya viongozi wa huku na baadhi ya WaTanzania kwamba maisha ni mazuri Tanzania na nhci imeendelea.
ReplyDeleteMzee wa Mtaa kwa Mtaa upo sawa kabisa:Kujenga kwenye mikondo ya maji ndio tatizo kubwa na inasabisha hasara na upotevu mkubwa wa rasilimali kidogo tuliyonayo. Lakini tufanyeje wachache kati yetu wanatumia uwezo wa kipesa na kuleta hasara kama hizo na kubaki kupiga kelele na mayowe.
ReplyDeleteWanaohusika warekebishe hali hii maji yapate njia na barabara iliyobomoka ijengwe ili isiharibike kabisa. Panaitaji kazi ya wataalamu katika sekta ya barabara watendaji fanyeni kazi.
ReplyDelete