Na Fredy Mgunda,Iringa
MATOKEO ya utafiti uliofanywa na taasisi ya Southern Highland Zone Election Research (SHZER), katika jimbo la Iringa mjini umeonyesha kuwa nyota ya Mwanahabari ,  Frank Kibiki aliyetangaza nia kuwania Ubunge jimbo la Iringa mjini (CCM) inazidi kung’ara baada ya kuongoza huku akichuana vikali na Mbunge wa sasa Mchungaji Peter Msigwa(CDM).
Utafiti huo uliofanywa kwa miezi minne tangu, kuwepo kwa wimbi la watu wengi kutangaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo la Iringa mjini, wakiwemo makada lukuki wa CCM unaonyesha kuwa Nyota ya Frank Kibiki inazidi kung’ara kutokana na kuungwa mkono na makundi mengi ya kijamii hasa vijana,  wanawake, walemavu na wazee.
Akizungumza na mtandao huu, Mtafiti mkuu wa SHZER,  Patson William alisema utafiti huo umefanywa katika kata 14 za jimbo la Iringa mjini huku wagombea vijana wakiwa ndio wanaoongoza kupendwa ikilinganishwa na wagombea wenye umri kuanzia miaka 50 na kuendelea.
Kibiki anaongoza kwa asilimia 40.7, Mchungaji Msigwa 20.9, Jesca Msambatavangu 11.7, Dr Yahaya Msigwa 7.6, Fredrick Mwakalebela 2.8, John Kiteve 2.4, Mahamoud Madenge 1.2 na wengine waliobaki wanagawana asilimia 12.7.
Utafiti huo unaonyesha kuwa, kinachomfanya Kibiki kuendelea kung’ara ni siasa zake za kistaarabu, taaluma ya uana habari, uwezo mkubwa wa kujenga na kujibu hoja anazokumbana nazo sambamba na uzoefu katika utendaji wake wakati akiwa Katibu wa UVCCM katika wilaya mbalimbali alizowahi kufanya kazi.
Alisema utafiti huo umefanywa kwa njia ya madodoso ambapo watu 400 walijibu na maswali ya papo kwa papo ambapo watu 1000 waliyajibu.
Alitaja kata zilizohusishwa kuwa ni Makorongoni, Miyomboni/kitanzini, Kihesa, Kwakilosa, Mlandege, Mivingeni, Gangilonga, Kitwiru, Igumbilo, Nduli, Ruaha, Mkwawa, Mtwivila na Isakalilo.
Mambo ya msingi ambayo utafiti huo uliangalia ili kutafuta majibu ni Changamoto za jimbo la Iringa mjini kwa sasa,sifa za Mbunge anayetakiwa kukabiliana na changamoto hizo, mapendekezo ya jina la atakayesimamia vizuri changamoto hizo na mazingira ya siasa za sasa za jimbo la Iringa mjini.
Hata hivyo CCM na Chadema ndiyo vyama pekee vinavyochuana kwa kasi katika jimbo la Iringa mjini, tangu CDM iliponyakua jimbo hilo mwaka 2010.
Hata hivyo utafiti huo unaonyesha kuwa CCM itakuwa na wakati mgumu ikiwa watateua jina la mtu asiyechaguo la wananchi jambo ambalo, litampa Mchungaji Msigwa ushindi usio na jasho.
“Utafiti huu unaonyesha kuwa CCM inanafasi nzuri ya kuchukua jimbo la Iringa mjini ikiwa tu watafuata nini wana Iringa wanasema vinginevyo, nafasi ya Msigwa kuendelea itakuwa kubwa,”anasema
       frank kibiki akiongea na wananchi stand kuu ya mabas iringa
 
wananchi wakimsikiza frank kibiki  alipokuwa maeneo ya stand kuu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 02, 2015

    Uwajibikaji na uhalali wa tafiti zinazotolewa na asasi ni vizuri uangaliwe na kusimamiwa ili usitumiwe kama njia ya kuharinbia wagombea wengine. Kama kuna taasisi ya habari/mawasiliano inayoweza kusimamia asasi zinazotoa matokeo na kufuatilia uhalali wa tafiti na matokeo yanayotolewa na asasi mbali mbali itasaidia kutoharibia wagombea wengine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...