Na Rahma Khamis – Maelezo
Zanzibar.
Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na azma yake ya kukamilisha Mradi wa Utafiti
wa Nishati mbadala ili kujuwa uwezekano wa Zanzibar kupata Umeme wake wa
uhakika.
Hayo
yameelezwa na Waziri wa Ardhi,Makazi,Maji na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban katika Ukumbi wa Baraza la
Wawakilishi Chukwani wakati akitoa Hutuba ya Makadirio ya Mapato
na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2015 /2016.
Amesema
Wizara yake imekamilisha kazi ya kupatikana
kwa Mkandarasi kutoka katika
Kampuni ya (AGMIN ya Italy) kwa Ujenzi wa Minara ambapo kwa sasa ameanza kazi
zake.
Aidha
amefahamisha kuwa Mshauri Elekezaji wa ukusanyaji wa taarifa pamoja na
kutaarisha Ripoti ya upembuzi sahihi (
Feasibility Study) ameshapatikana ambapo kazi yao inatarajiwa kumalizika Mwaka
( 2017)
Itakumbukwa
kuwa Zanzibar bado inategemea Nishati ya Umeme kutoka Tanzania Bara na kwamba
kama Utafiti huo utatoa Matokeo mazuri kuna uwezekano wa Zanzibar kuwa na
Vyanzio vyake vya Umeme badala ya kutegemea Bara.
Waziri Shabani
amesema katika utekelezaji huo Wizara imeweza kushiriki katika mikutano
mbalimbali iliyofanyika ndani na nje ya Nchi ikiwemo kuhudhuria katika mkutano
wa kuitangaza Tanzania katika utekelezaji wa masuala ya Nishati (Den
Hague-Uholanzi).
Akielezea kuhusu
utekelezaji huo amesema kuwa ni
kushiriki katika Maonesho na Warsha ya Nishati Mbadala iliyo fanyika Kahama na
Tanzania, na kushiriki Vikao vya Jumuia ya Afrika Mashariki katika masuala ya
Nishati na Umeme (Nairobi Entebe) sambamba na mkutano mkuu wa Mafuta na Gesi wa
Afrika Mashariki (EAPCE 2015) uliofanyika Kigali –Ruwanda.
Hata hivyo
amesema katika kuhakikisha Nishati ya Mafuta inapatikana Nchini Wizara
inaendelea kufuatilia shughuli za kusimamia upatikanaji wa Mafuta pamoja na
utekelezwaji wa Ratiba za uagizaji wa Mafuta Nchini kwa Makampuni manne makubwa
(GAPCO,UP,ZP na PUMA).
Aidha amefahamisha kuwa katika kulisimamia suala
hilo dosari za uagizwaji wa Mafuta ya Petrol zimejitokeza baina ya Mwezi wa
Februari na Machi ambazo zilichangiwa na kuchelewa kwa Meli ya Mafuta ya pamoja
(Bulk Consignment) inayoleta Mafuta Nchini Tanzania.
Sambamba na hayo Waziri Shaaban amesema kutokana na
hali iliyojitokeza ni kiashirio tosha cha kusisitiza umuhimu wa kuwepo kwa
Taasisi maalum ya kushuhulikia Sekta Binafsi ya kuendesha Biashara hiyo kwa
kutumia sheria.
Waziri Shaaban
ameliomba Baraza la Wawakilishi limuidhinishie Jumla ya Shl. Bilion 35 na
Milioni 949 kwa ajili ya Wizara ya Ardhi Makaazi Maji na Nishati kwa mwaka wa
Fedha 2015-16.
IMETOLEWA
NA HABARI MAELEZO –ZANZIBAR.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...