Na Mwandishi wetu
Vijana wameridhishwa na mswada uliopitishwa bungeni wa kuanzishwa baraza la vijana la Taifa
na kudai kuwa hiyo ndio njia mojawapo vijana wanaweza kuendeleza shughuli zao za maendeleo
.
Wamedai kuwa katika mswada huo vijana wanangazi zao za uongozi kutoka vijijini hadi kitaifa na
hali hiyo inakuwa ni rahisi vijana kuwa na uwezo wa kuelezea changamoto zinazowakabili .
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na shirika la Restless Development Tanzania – ICS)
linalojishughulisha na kuwaweka vijana kuwa mstari wa mbele katika kufikia maendeleo mara
baada ya kumalizika kwa sherehe ya kutoa vyeti kwa vijana wakujitoea ambao wanasoma katika
vyuo vikuu .
Mkurugenzi wa ICS bibi Margareth Mriwa alisema wamefurahishwa na mswada wa baraza la
vijana kupitishwa bungeni na kudai kuwa wanaamini kwamba katika muswada huo kuna mikakati
inayofaa kabisa ya kuwaelekeza vijana kufikia maendeleo .
‘’ Kwasasa hivi waliowengi nchini Tanzania ni vijana na wanauwezo wa kuchangia maendeleo na
tunaomba wapewe fursa hiyo katika ngazi mbali mbali za maendeleo . Jambo la kwanza ni
kwamba vijana wamejitenga kidogo katika jamii zao na hawapati nafasi wanazopenda
kuchaguliwa ‘’ alisema bibi Margareth .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...