Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya biashara ya
DCB Bw. Samwel Dyano akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo Balozi Paul
Rupia hayupo pichana juzi jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa
filamu ya Desire to Succeed iliyodhaminiwa na benki hiyo kwa lengo la
kuhamasisha jamii kutumia huduma za kibenki katika kuyafikia mafanikio yao.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB,
Balozi Paul Rupia akizungumza wakati wa
hafla ya uzinduzi wa filamu ya Desire to Succeed juzi jijini Dar es
Salaam.Filamu hiyo imetengenezwa na ya Kampuni ya Consnet Group Ltd ya jijini
Dar es Salaam kufuatia udhamini wa DCB Benki ikiwa ni njia ya kujitangaza.
Mwakilishi wa Kampuni ya Consnet Group ambayo ndiyo
waandaaji wa filamu ya Desire to Succeed Bw. Sanctus Mtisimbe (mwenye tai
nyekundu) akiwatambulisha baadhi ya wasanii (wahusika) muhimu walioshiriki
katika filamu hiyo juzi jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa
filamu hiyo iliyoambatana na futari chini ya udhamini wa Benki ya Biashara ya
DCB.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi.
Joyce Fissoo akitambulishwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa filamu ya Desire to
Succeed iliyodhaminiwa na benki hiyo kwa lengo la kuhamasisha jamii kutumia
huduma za kibenki katika kuyafikia mafanikio yao.
Baadhi ya wasanii waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa
filamu ya Desire to Succeed wakijitambulisha juzi jijini Dar es Salaam.Filamu
hiyo iliyodhaminiwa na benki ya Biashara ya DCB.
Kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
Tanzania Bibi. Joyce Fissoo, msanii Rose Ndauka, Tito Mrisho Zimbwe na
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara ya DCB Balozi Paul Rupia
wakionyesha DVD ya filamu ya Desire to Succeed juzi jijini Dar es Salaam mara baada
ya kuzinduliwa rasmi. Filamu hiyo imetengezwa na kampuni ya Consnet Group chini
ya udhamini wa DCB Benki ikiwa ni njia ya kujitangaza kupitia ubunifu wa sanaa
ya filamu.
Picha na Frank Shija, WHVUM. Kwa habari kamili BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...