Mratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka, akifafanua juu ya Umuhimu wa Tathmini ya Hali ya Chakula na Lishe nchini wakati Wataalam na waratibu maafa mkoani Shinyanga walipokuwa wakijifunza uendeshaji wa tathmini hiyo katika kijiji cha Uzogore mkoani humo
Wataalam na waratibu maafa mkoani Shinyanga wakijifunza kwa vitendo uendeshaji wa Tathmini ya Hali ya Chakula na Lishe nchini katika kijiji cha Uzogore mkoani Shinyanga, mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu
Mwanakijiji cha Uzogore, Mkoani Shinyanga, akitumia mawe kufafanua uwiano wa Hali ya Chakula na Lishe kijijini hapo wakati Wataalam na waratibu maafa mkoani humo wakijifunza kwa vitendo uendeshaji wa Tathmini ya Hali ya Chakula, mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu
Mratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Theodosia Mbunda akipongezwa na wanakijiji cha Uzogore, Mkoani Shinyanga, mara baada ya kuwaeleza umuhimu wa Hali ya Chakula na Lishe kijijini hapo wakati Wataalam na waratibu maafa mkoani humo walipojifunza kwa vitendo uendeshaji wa Tathmini hiyo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...