wafanyakazi wa Hoteli ya Dar es Salaam Serena ambao ni wakereketwa
wakubwa wa mazingira, waliadhimisha siku hii asubuhi ya leo kwa kufanya
usafi barabara ya Ohio kuzunguka
mpaka ufukwe wa bahari ya Hindi.
Akiongea mara baada ya zoezi hilo la usafi mkurugenzi mkuu wa masoko wa
hoteli hiyo ndugu Seraphin Lusala aliwashukuru wafanyakazi wa hoteli
hiyo kwa kushiriki katika zoezi hilo la kufanya usafi wa mazingira ili
kuonyesha mfano kwa jamii
kwamba uchafuzi wa mazingira haukubaliki na kuwataka wafanyakazi wa
hoteli hiyo kuwa mfano hata huko wanapoishi kwa kutokutupa taka hovyo na
kuwaelimisha wale wanaotupa taka hovyo na kuchafua mazingira kuacha
tabia hiyo ili kufanya mazingira yetu na jiji letu
kuwa safi.
wafanyakazi wa Hoteli ya Dar es Salaam Serena ambao ni wakereketwa wakubwa wa mazingira wakiendelea na zoezi la usafi kando ya barabara ya Ocean Road, jijini Dar katika kuadhimisha siku ya Mazingira.
wafanyakazi wa Hoteli ya Dar es Salaam Serena ambao ni wakereketwa wakubwa wa mazingira wakiwa katika picha ya pamoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...