Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Kanda ya Ziwa Bwa.Mugisha Murshad wakati alipokuwa akitoa malalamiko ya wafugaji kwa ukatili wanaofanyiwa na askari wa wanyamapori katika mapori mbalimbali ya hifadhi kanda ya ziwa.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa wafugaji wamekuwa wakifunga safari kwenda mkoani Dodoma kwa ajili ya kuonana na mawaziri wahusika akiwemo, Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dk.Titus Kamani , aliyekuwa Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka na Waziri Mkuu Pinda.

Pia alisema wamefanya vikao kati yao na wakuu wa wilaya za mkoa wa Kagera pamoja na Mkurugenzi wa Wanyamapori lakini hakuna kilichoifanikiwa zaidi ya kupewa tarehe ya kwamba ufumbuzi utapatikana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma taarifa ya vikao 17 vilivyofanyika kati ya Wafugaji hao (pichani)  na viongozi mbalimbali  wa Serikali,kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa mgogolo wao dhidi ya Askari wanyama pori lakini hakuna maamuzi ama suluhisho lililopatikana.Kinana amekutana na wafugaji hao mapema leo katika kijiji cha Nyakanazi wilayani Biharamulo na kutoa kero zao kwake juu ya manyanyaso wanayofanyiwa na askari wa wanyamapori.

Alisema kuna mambo mawili yamemsikitisha, moja watu kutumia mwamvuli wa sheria kufanya mambo yao binafsi kwani hakuna Serikali inayoweza kutumbukiza ng'ombe kwenye shimo.

"Wizi ,rushwa ndicho kinachoonekana ndani yake, kwa maelezo yenu kuna baadhi ya watendaji wameamua kuchukua sheria mkononi mwao.Wanachukua milioni 10 za mfugaji na kisha zinakwenda kwenye mifuko yao,"alisema.

Alisema lazima akiri, Serikali nayo imelegea mno katika kuchukua maamuzi, kwani amehesabu vikao ambavyo wafugaji wamekaa na viongozi wa ngazi mbalimbali za juu serikali vipatavyo 17 lakini hakuna ufumbuzi na badala yake ni maneno, maneno tu.

Alisema kama wameshindwa kutatua matatizo ya watu ni vema wakaa kando maana mishahara wanalipwa na marupurupu wanapewa lakini kushughukulikia matatizo ya watu imekuwa ngumu.

"Watu wameuawa, ng'ombe wamekufa, ng'ombe wameporwa.Hii haiwezekani na kwamba matatizo yote yanayohusu wanyamapori wenye mamlaka ni Wizara ya Maliasili na Utalii.

"Niombe mambo mawili yafanyike, ng'ombe waliokamatwa warudishwe kwa wafugaji na pili kesi zilizopo mahakamani zifutwe na wenye mamlaka ya kuzifuta ni Serikali maana ndio waliofungua kesi,"alisema Kinana.
Baadhi ya wafugaji wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati alipokuwa akizungumza nao katika kijiji cha Nyakanazi Wilayani Biharamulo mkoani Kagera.Kwa mujibu wa wafugaji hao wameeleza kuwa wilaya zote zilizopo Mkoa wa Kagera na hasa Wilaya ya Ngara , wafugaji wamekuwa wakipata mateso makubwa pindi mifugo yao inapokamatwa kwenye pori la Kimisi ambapo ng'ombe wamekuwa wakipigwa risasi na wengine kuingizwa kwenye shimo refu lenye tope linalojulikana kwa jina la Gwantanamo.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Kanda ya Ziwa Bwa.Mugisha Murshad wakati alipokuwa akimuonyesha eneo linalotumika kuhifadhi mifugo yao mara inapokamatwa na kuwa eneo hilo ni dogo na halina chakula cha mifugo wala maji jambo ambalo hupelekea mifugo kufa kwa wingi.
Mmoja wa wafugaji akimuonesha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana eneo ambalo mifugo inayokamatwa hupelekwa hapo na kuwekwa kwa muda mrefu bila maji wala chakula na matokeo yake mifugo hufa,iwapo mwenye mifugo hiyo hakwenda kuikomboa kwa gharama itakayokuwa imetajwa,ambayo wafugaji hao wamekuwa wakiilamimikia 
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akioneshwa eneo ambalo mifugo ya Wafugaji ilikuwa ikikusanywa eneo hilo na kuacha kwa muda mrefu bila chakula wala maji na hatimae kupoteza uhai,jambo ambalo wafugaji hao wameona ni kitendo cha uonevu na unyanyasaji mkubwa,kwani kwa kukamatwa mifugo yao wamekuwa wakitozwa fedha nyingi kuikomboa mifugo yao,hivyo wameomba Ndugu Kinana kusikiliza kilio chao cha mda mrefu. MICHUZI JR-KAGERA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...