Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imesema maboresho mbalimbali yanayofanyika kwenye Bandari ya Dar es Salaam na kuimarishwa kwa mahusiano na wadau wake vimesaidia kuongeza ufanisi bandarini. 
 Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Bw. Awadhi Massawe alisema mahusiano mazuri ya kikazi na wadau pamoja na uboreshaji wa miundombinu na huduma vimechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza ufanisi bandarini. 
 “Wahariri na waandishi wa habari mnamchango mkubwa sana kwa maendeleo ya bandari ya Dar es salaam na nyingine zilizopo chini ya mamlaka,” alisema na kuongeza kuwa kwa sasa ukuaji wa mzigo unapita Bandari ya Dar es salaam ni asilimia 14 kwa mwaka. 
 Bw.Massawe alikutana na wahariri hao ikiwa ni miezi mitatu tu tangu alipoteuliwa kukaimu nafasi, alisema tasnia ya habari in mchango mkubwa sana katika kuchochea maendeleo na hivyo bandari kama lango kuu la uchumi ni vyema ikafanya kazi kwa karibu iliwafamisha wadau na watumiaji wa bandari juu ya maendeleo na maboresho mbalimbali yanayoendelea kwa faida ya nchi. Alisema TPA itaendelea kudumisha mahusiano na wadau wote vikiwemo vyombo vya habari ili kuweza kuleta tija ya uboreshaji pamoja na ufanisi katika bandari za Tanzania
 Akifafanua zaidi kuhusu maboresho ya bandari, Bw. Massawe alisema kuwa bandari inachangia kwa kiasi kikubwa cha mapato ya serikali kupitia kodi inayokusanywa na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA). “Wastani wa asilimia 40% ya mapato ya TRA yanatoka Bandari ya Dar es Salaam,” alisema Bw. Massawe 
Aliongeza kuwa bandari ni lango kuu la uchumi na hiyo ushirikiano na wadau wake utaongeza zaidi ufanisi. 
 Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri nchini, Bw.Absalom Kibanda, ambaye pia ni Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari Corporation, alisema kuwa kuna umuhimu wa bandari kuweza kusaidia kifedha wadau mbalimbali kama TAZARA na shirika la Reli la Tanzania ni hatua nzuri sana ambapo itaweza kuongeza ufanisi wa reli katika bandari. 
 “Hii italeta ufanisi mkubwa sana katika usafirishaji wa mizigo kutoka bandarini kwenda maeneo husika,”alisema Bw. Kibanda. 
 Naye Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Nipashe Bw. Jesse Kwayu alisema kuwa ni juuhudi kubwa ambayo imefanyika katika kuboresha huduma za bandari na hivyo ni vizuri kuboresha miundombinu ya nje kama njia ya reli na barabara ili huduma za usafirishaji wa mzigo ziweze kwenda kwa kasi zaidi. 
 “Kuna umuhimu wa kufufuliwa kwa njia ya reli pamoja na upanuzi wa barabara ili ufanisi wa bandari uweze kuwa na faida kubwa na kuongezeka kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi yetu,” alisisitiza Bw. Kwayu.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi Bandari Tanzania(TPA), Bw. Awadhi Massawe akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, ambapo moja ya ajenda ilikuwa kufahamiana na kuwaendelea hatua na mikakati iliyochukuliwa na mamlaka katika kuongeza ufanisi kwenye Bandari ya Dar es Salaam.  kulia ni  naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo (Huduma), Bw. Rajah Mdoe.
 Sehemu ya wahariri katika kikao hicho
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi Bandari Tanzania(TPA), Bw. Awadhi Massawe, akimkabidhi zawadi Naibu Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali(Dailynews, Habari Leo), Bi.Tuma Abdallah, mara baada ya  mkutano wake na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, ambapo moja ya ajenda ilikuwa kufahamiana na kuwaelezea hatua na mikakati ilizochukuliwa na mamlaka katika kuongeza ufanisi kwenye Bandari ya Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa  Bandari Tanzania(TPA), Bw. Awadhi Massawe akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri ambaye pia ni Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari Corporation, Bw. Absalom Kibanda mara baada ya mkutano wake na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, ambapo moja ya ajenda ilikuwa kufahamiana na kuwaelezea hatua na mikakati ilizochukuliwa na mamlaka katika kuongeza ufanisi kwenye Bandari ya Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi Bandari Tanzania Bw. Awadhi Massawe akimkabidhi zawadi Mhariri mtendaji wa magazeti ya uhuru na mzalendo Bw. Joseph Kulangwa, mara baada ya  mkutano wake na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, ambapo moja ya ajenda ilikuwa kufahamiana na kuwaelezea hatua na mikakati ilizochukuliwa na mamlaka katika kuongeza ufanisi kwenye Bandari ya Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Bw. Awadhi Massawe akimkabidhi zawadi Kaimu Mhariri Mkuu (Habari leo), Bw.Nicodemus Ikonko, mara baada ya mkutano wake na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, ambapo moja ya ajenda ilikuwa kufahamiana na kuwaelezea hatua na mikakati ilizochukuliwa na mamlaka katika kuongeza ufanisi kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...