Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi amemaliza ziara ya siku mbili Mkoani Lindi ambapo alikagua shughuli za Shirika la Nyumba la Taifa na kusikiliza migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi wa Lindi eneo la Mitwero na kuitatua.
Katika ziara hiyo, Waziri Lukuvi amewaonya na kuwaagiza Maafisa ardhi, wapima na maafisa mipango miji kuacha mara moja kujinufaisha kwa kuwadhulumu wananchi haki zao za ardhi.
Aidha ameutaka Mkoa wa Lindi kuharakisha upimaji wa ardhi ya wananchi na utoaji wa hati ili kuwawezesha wananchi kumiliki ardhi na kupunguza migogoro ya ardhi.
Waziri William Vangimembe Lukuvi akisisitiza jambo baada ya Watendaji wa sekta ya ardhi ya Mkoa wa Lindi kushindwa kumudu maswali mbalimbali aliyowauliza na kuwataka watendaji hao kujipima kama bado wanastahili kuendelea kuwatumikia wananchi kwa nafasi zao wanazotumimkia.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Mwantumu Mahiza akimuomba Mheshimiwa William Lukuvi kuwaondoa watendaji wabovu wa sekta ya ardhi Mkoani Lindi akisema kuwa wapo watanzania wengi wenye uwezo wa kufanya kazi zao. Alisema kuwa hayuko tayari kuyumbisha kiti chake alichoaminiwa na Rais kwa kuwalea watendaji wazembe.
Sehemu ya umati wa wananchi waliofika eneo la Mitwero kuwasilisha kero zao kwa Waziri William Lukuvi. Malalamiko mengi ya wananchi yanatokana na kutokushirikishwa katika uthamini wa ardhi na mali yao hali ambayo imewafanya kupunjwa malipo ya fidia. Waziri Lukuvi ameagiza wanaothamini mali ya wananchi kote nchini kufanya kazi hiyo kwa uaminifu na kuwashirikisha wananchi hao katika hatua zote ili kuondoa malalamiko na kutenda haki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...