Mjumbe wa Bodi ya Filamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bi.Vicensia Shule(wa kwanza kutoka kushoto) akimwuliza  jambo Mwenyekiti wa makampuni ya Proin Bw,Johnson Lukaza(hayupo pichani) leo jijini Dar es salaam walipotembelea kujionea  miundombinu ya kampuni hiyo.Kutoka kulia ni Makamu mwenyekiti wa  wa Bodi iyo Bw.Sylvester Sengerema na katikati ni  Bw.Bishop Hiluka.
 Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi,Joyce Fissoo akichangia jambo wakati walipotembelea miundombinu ya Filamu ya Makampuni ya Proin.Bi Fissoo ametoa wito kwa makampuni yanayotengeneza Filamu Tanzania kuendelea kushirikiana na Serikali ili kuimarisha Tasnia ya Filamu na kusaidia katika kupambana na Changamoto mbalimbali.
Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Bw,Johnson Lukaza akimwonyesha Katibu mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi,Joyce Fissoo  moja ya Kazi walizotengeneza na kuingia Sokoni,Pia aliiomba Serikali kusaidia kuweka sheria kali zitakazo zuia wizi wa Filamu nchini.
Wajumbe wa Bodi ya Filamu Tanzania wakifurahia jambo na Mkurugenzi wa Makampuni ya Proin Bw,Johnson Lukaza(wa tatu kutoka kushoto) walipotembelea miundombinu ya kutengenezea filamu ya Kampuni iyo eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam.Wajumbe hao walijionea jinsi Filamu inavyotengenezwa na pia walitembelea eneo kampuni iyo wanapojenga Studio ya kutengenezea Filamu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...