Mlezi wa Shule ya Msingi Kiluvya ‘B’, Kanali Thomas Ndonde (wa pili kulia), akimkabidhi hati ya utambuzi wa ushirikiano wa maendeleo baina ya shule hiyo na wataalamu wa Jeshi la Ukombozi wa China, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Ziada Libaba wakati wa hafla ya kukabidhiwa misaada yenye thamani ya ShMilioni 3, iliyofanyika shuleni hapo jana.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kiluvya ‘B’, Ziada Libaba akikabidhiwa moja ya kompyuta mpakato kutoka kwa Kiongozi wa msafara wa wapiganaji wa Jeshi la Ukombozi wa China, Zhao Batao ambao walitoa msaada wenye thamani ya Zaidi ya Sh3 Milioni, katika hafla iliyofanyika shuleni hapo, Kisarawe Pwani jana.
Mlezi wa Shule ya Msingi Kiluvya ‘B’, Kanali Thomas Ndonde (wa tatu kulia), akimkabidhi sehemu ya msaada wa vitabu kutoka kwa wapiganaji wa Jeshi la Ukombozi wa China, Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kiluvya ‘B’, Ziada Libaba hafla iliyofanyika, shuleni hapo Kisarawe jana.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta), wakilifanyia marekebisho moja kati ya magari mawili yaliyotolewa na wahisani wa Shirika la Misaada ya Marekani (USAID), katika karakana yao Chang’ombe jijini Dar es Salaam jana. Picha na Joseph Zablon.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...