Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe. Jenista Mhagama (mwenye nguo nyekundu) akimfariji Mwenyekiti wa Bunge Bi. Lediana Mng’ong’o mara baada ya bunge kuahirishwa kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Ukonga Bi. Eugen Mwaiposa. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora Bi. Mary Nagu na kushoto ni wabunge James Mbatia na Goodluck Ole Medeye.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Anjela Kairuki (kushoto) akitoka nje ya ukumbi wa bunge akiwa ameambatana na wabunge Bi. Mary Mwanjelwa na Rita Kabati baada ya bunge hilo kuahirishwa kufuatia kifo cha Mbunge wa Ukonga Bi. Eugen Mwaiposa.
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ukonga marehemu Bi. Eugen Mwaiposa ambaye amefariki usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake mjini Dodoma. Taarifa za kifo chake zimetangazwa wakati bunge likiendelea na mjadala wa bajeti ya wizara ya afya hivyo kupelekea bunge hilo kuahirishwa hadi tarehe 4 mwezi huu.
Baadhi ya wabunge wakiwa kwenye hali ya simanzi baada ya kutangazwa kifo cha aliyekuwa mbunge wa Ukonga Bi. Eugen Mwaiposa kilichotokea usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake mjini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 02, 2015

    Pole sana wana familia, lakini bongo wakati wa kukaribia uchaguzi wabunge na viongozi huwa wanafariki katika mazingira ya ajabu.Wengine wanatumia wakati huu kujipanga kutaka kuchukua kiti chake kwa gharama yoyote ile.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...