Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Mbeya, wakiwa wamemzunguka, Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa (katikati), wakati alipowasili kwenye Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya leo Juni 19, 2015, kukabidhiwa fomu zitakazomuwezesha kupata ridhaa ya Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mbeya wamevunja rekodi udhamini kwa Mh. Lowassa ya mikoa yote aliyopita, amepata wadhamini 53,156 kwa mkoa wa Mbeya pekee.
PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipunga mkono kwa Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Mbeya, waliofurika kwa wingi wao kwenye Uwanja wa Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya, wakati alipowasili kwenye Ofisi hizo leo Juni 19, 2015, tayari kwa kupokea fomu za WanaCCM 53,156 wanaliomdhamini ili apate ridhaa ya Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza machache na kutoa shukrani kwa WanaCCM na Wananchi wa Mkoa wa Mbeya waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya, leo Juni 19, 2015.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za WanaCCM zaidi ya elfu tisa wa Wilaya ya Mbeya Vijijini kutoka kwa Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo, Mary Kalinze.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...