Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiwapungua mkono WanaCCM wa Mji wa Kibaha Mjini wakati alipofika kwenye Ofisi za CCM kukabidhiwa orodha ya majina ya WanaCCM waliomdhani ili apate ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Jumla ya WanaCCM 78, 500 wamdhamini Mh. Lowassa, Mkoani Pwani.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.

Katibu wa CCM Wilaya ya Temeke, Abdallah Mdimu akikabidhi fomu yenye orodha ya majina ya Wadhamini kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa leo Juni 28, 2015. Jumla ya WanaCCM 78, 500 wa Mkoa wa Pwani Wamemdhamini Mh. Lowassa ili apate ridhaa ya CCM kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Askofu mstaafu wa Kanisa kuu la KKKT Dayosisi ya Dodoma, Peter Lukumbusho Mwamasika akimuombea Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, wakati alipofika kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Kibaha Mjini kukabidhiwa orodha ya majina ya WanaCCM waliomdhamini kugombea Urais wa Tanzania, leo Juni 28, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiwaralimia Watoto, Aisha (12) na Sikuzani (4) waliomfata kumsalimia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...