Mzee wa CCM wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Yusuf Bundala Kasubi, (kulia), akimkabidhi Waziri Mkuu wa Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, zaidi ya shilingi milioni moja, zilizochangwa na wanachama wa CCM mkoani Tabora, ili azitumia kulipia ada ya kuchukua fomu za kuwania urais kupitia chama hicho. Hafla ya kukabidhi fedha hizo ilifanyika nyumbani kwa Mtangaza nia huyo, mjini Dodoma leo Alhamisi Juni 4, 2015.
Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Majaliwa Bilali, (kulia), akizungumza sababu zilizowapelekea wana CCM mkoani humo kuchanga fedha za kumuwezesha Mtangaza nia ya kuwania urais kupitia CCM, Waziri Mkuu wa mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, (kushoto), wakati wa hafla fupi ya kukabidhi mchango huo wa zaidi ya shilingi milioni 1 zilizofanyika nyumbani kwa mtangaza nia huyo, mjini Dodoma, Alhamisi Juni 4, 2015.
Waziri Mkuu wa mstaafu na Mbunge wa Monduli, ambaye tayari ametangaza nia ya kuwania urais kupitia CCM, Edward Lowassa, akiwashukuru wana CCM kutoka mkoani Tabora, baada ya kumkabidhi mchango wao wa zaidi ya shilingi milioni 1 ili azitumie kulipia ada ya kuchukua fomu za kuwania urais katika hafla iliyofanyika nyumbani kwake mjini Dodoma, leo.
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, ambaye tayari ametangaza nia ya kuwania urais kupitia CCM, Edward Lowassa, akisalimiana na ujumbe wa wana CCM kutoka mkoani Tabora, walipofika nyumbani kwake mjini Dodoma leo Alhamisi Juni 4, 2015, ili kumpatia mchango wao wa nkumuwezesha kulipia ada ya fomu ya kuwani urais.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...