Na Woinde Shizza,Arusha
Wito umetolewa kwa wazazi kutumia mda mwingi kukaa na watoto wao ili kuwaepusha na vishawishi mbalimbali ambavyo wanaweza kuvipata.

Hayo yamebainishwa na  Afisa ustawi wa jamii wa jiji la Arusha Saumu

kweka wakati akiongea na wazazi ,walimu  na wanafunzi juu ya adhari
zinazoweza kumapata mtoto wakati kipiondi ambacho autaweza kuwa nae.

Alisema kuwa kumtelekeza mtoto kunaweza kusababishia vitu vingi

vikiwemo mimba za utotoni kwa upande wa watoto wa kiume kulawitiwa
pamoja na kujifunza tabia chafu ambazo zinamuharibu mtoto huyo.


Alisema kuwa kumekuwa nawazazi wengi wamekuwa  wanafanya wafanyakazi wa ndani kama walezi hali ambayo inapelekea watoto kujifunza tabia chafu kwani wasichana wengi wamekuwa hawawafatilii watoto vizuri kama jinsi mzazi ungekuwa unamfatilia.

“unakuta kipindi hichi wazazi wengi wanajidai wapo bize kutafuta hela

hawezi ata kumuangalia mtoto  hawezi kufatilia mwenendo ya mtoto kitu
ambacho mtoto inafikia mahali anafanya kitu anachokitaka  na hii
inapelekea kwa mfano mtoto wa kike umemuacha umfatiliii wewe uko
kazini umemuacha na mfanyakazi w akiume anaweza kumfanya chochote au
pia mtoto unamuacha anazurura anaweza kukutana na wababa huko
akawadanganya na vichipsi mayai akaenda na mtoto sababu ukai na mtoto
ukampa maitaji anayoyataka sasa akienda kupew achipsi uko utajua
mwishowe ndio unaletea mimba nyumbani saa nyingine watoto wa kiume
ndio wanakuw amashoga”alisema saumu.


Aidha aliwataka wazazi ambao ni wakali kupunguza ukali kwa watoto wao

ili iwapo mtoto atafanyiwa kitu chochote au atakubwa na kitu chochote
iwe rahisi kumuelezea mzazi kwani kuna wazazi wengine wanakuwa wakali
mpaka watoto wanashindwa kuwaeleza matatizo ambayo wanayo.


Kwa upande mwalimu mmoja wapo aliyejitambulisha kwa jina la Gwantu

Mwakabungu aliwaomba wazazi wenyehela kupunguza kuwapa fedha nyingi
watoto wao kwani kitendo cha kuwapa fedha nyingi watoto wao
kinawapelekea waatoto kuwa na zarau hata kwa walimu wao kutokana na
fedha walizo nazo.

Aidha aliiomba serekali kuunda sheria ambayo itazuia wanafunzi kuwa na
simu mashuleni na hata manyumbani kwani kwa kufanya hivyo itasaidia
kupunguza mmonyoko wa maadili kwani simu nyingi zimekuwa zikiwapotosha wanafunzi wengi.

Afisa ustawi wa jamii  jiji la Arusha Saumu kweka akiwa anaongea  katika mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2015

    Malezi ni muhimu, kuachia wafanyakazi wenye uelewa mdogo na ambao ni wadogo wanaohitaji kulelewa ni changamoto pia. Ndugu wanaweza kusaidia kukaa iwapo mzazi lazima aende kazini au shambani lakini wapo nao wenye upungufu. Ni vizuri kuwa macho na kufuatilia. Kazi za ndani zitakapokuwa ajira rasmi zikifanywa na watu wazima kama Afrika Kusini zikiwa na taratibu na maslahi kama kazi zingine saa za kazi na siku ya kupumzika zitakuwa na uwajibikaji zaidi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...