



Mwanafunzi Yahya Mhata ambaye kwa pamoja wamebuni mfumo huo, ameuelezea kuwa ni mzuri na rafiki wa mazingira huku ukiweza kuhifadhi kumbukumbu za mawasiliano kwa uhakika tofauti na ule wa kadi za makaratasi ambao wengi hupoteza kadi hizo na kujikuta wakipoteza mawasiliano muhimu.
Wanafunzi wengine wa Shule za Fedha ambao ni Prince Mwemezi Muzamil Katunzi, Goodluck Komba, Sajjad El-Amin na Veronica Samuel Ndomba ambao kila mmoja ameshinda medali za fedha katika makundi ya ushindani tofauti chini ya usimamizi wa mwalimu Metin Er wa Masomo ya Biashara, Fedha International School walieleza kunufaika na mashindano kitaaluma na upeo.
Mwanafunzi Mwemezi Muzamil Katunzi, ambaye aliwasilisha picha yenye ujumbe wa mazingira na kushinda alisema picha hiyo aliipiga eneo la viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam ikielezea namna binadamu wanaathiri mazingira kwa kuchoma moto hovyo na kuleta matatizo mengine duniani. Kwa upande wao wanafunzi Goodluck Komba na Sajjad El-Amin waliwasilisha andiko la mradi wa kutengeneza mkaa kwa kutumia makaratasi taka ambao ulishika nafasi ya tatu katika mashindano ya Genius Olympiad yaliyofanyika jijini New York.
Mwanafunzi Komba alisema mradi wao ni rafiki wa mazingira na ukitumika utaokoa sehemu kubwa ya uharibifu wa mazingira. Kwa upande wake msichana pekee aliyeshinda katika mashindano hayo, Veronica Samuel Ndomba alisema andiko lake lilishinda kwenye kipengele cha 'Mazingira Yetu' na aliandika kuonesha namna elimu ya mazingira inaweza kutolewa na kulinda uharibifu mkubwa wa mazingira unaofanywa katika shughuli mbalimbali za binadamu.
Naye msimamizi wa wanafunzi hao, mwalimu Metin Er alisema kundi hilo la wanafunzi mbali na kujijenga kimaarifa kwa wanafunzi hao wameiletea sifa Tanzania kwani kwani mashindano hayo ya kitaaluma yalishirikisha nchi mbalimbali zikiwemo USA, Romania, Nigeria, Tunisia, Holland, Turkmenistan, Kazakhstan and Russia. Shule za Fedha International School zimekuwa zikifanya vizuri kitaaluma kitaifa na kimataifa jambo linaloendeleza umaarufu wa shule hizo kila uchao. *Imeandaliwa na www.thehabari.com
Hapa naamini sasa serikali ya Tanzania haipo tayari kuboresha mfumo wa elimu kwa masikini.utajiuliza kivipi nasema hivyo ,,,!!! Ila tafakari hapo juu Na namna Watoto wetu wa kimasikini wanavyoshindwa kuwa Na elimu bora inayo endana Na mwendo Kasi wa dunia.nilitamani kuona wanafunzi hasa watokee shule za kata. Mfumo wa elimu wa Tanzania yetu Ni sawa Na pyramid .
ReplyDelete