MAHAKAMA YA TANZANIA YAKUTANA NA UJUMBE KUTOKA BENKI YA DUNIA PAMOJA NA
WADAU WENGINE WA MAHAKAMA KUJADILI JUU YA MABORESHO YA HUDUMA YA UTOAJI
HAKI NCHINI

Meza Kuu ikiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Mahakama kutoka Wizara
ya Katiba na Sheria, Chuo cha Sheria, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, na baadhi ya Wawakilishi kutoka REPOA na wengineo walioshiriki
katika Warsha kati ya Mahakama, Ujumbe wa Benki ya Dunia na Wadau wa
Utoaji haki juu ya uboreshaji wa utoaji huduma za Mahakama na kusogeza
huduma za Mahakama karibu na wananchi.
Mhe. John Kahyoza, Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania akitoa mada juu
ya Maboresho yanayoendelea kufanyika ndani ya Mahakama ya Tanzania kwa
washiriki wa Warsha hiyo.
Washiriki wa Warsha hiyo wakisikiliza mada inayotolewa juu ya Maboresho
ya Mahakama, moja Kati ya maeneo yaliyojadiliwa katika kuleta maboresho
ni pamoja na Kurahisisha upatikanaji wa haki, kuboresha utawala wa
Mahakama, kuimarisha Imani ya wananchi kwa Mahakama, na Ushirikishwaji
wa wadau katika kuboresha huduma za Mahakama. (Picha na Mahakama ya
Tanzania).
![]() | |||
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...