000000
 Msanii maarufu wa vichekesho nchini wa Kundi la Kashi-Kashi anayeshiriki katika kipindi cha Mizengwe cha Kituo cha ITV, Habib Mrisho (Sumaku) akisaini kitabu cha wageni katika banda la Jeshi la Magereza wakati msanii huyo na mwenzake Jesca Kindole kwa jina maarufu la uigizaji (Safina -kulia) walipotembelea mabanda ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kulia ni maafisa wa Jeshi hilo.
00000
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Bulimba (kulia) akiwapa maelezo wasanii maarufu wa vichekesho wa Kundi la Kashi-Kashi wanaoshiriki katika kipindi cha Mizengwe cha Kituo cha ITV, kuhusu taarifa mbalimbali zinazoandaliwa na Jeshi hilo, katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Jesca Kindole (Safina) na Habib Mrisho (Sumaku).0000
 Wasanii maarufu wa vichekesho nchini wa Kundi la Kashi-Kashi wanaoshiriki katika kipindi cha Mizengwe cha Kituo cha ITV, wakipewa maelezo na Koplo wa Jeshi la Polisi, Sylvester Mganga, kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Jeshi hilo, katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Habib Mrisho (Sumaku), Jesca Kindole (Safina) na Rashid Costa (Maringo 7).000
2. “UTII WA SHERIA BILA SHURUTI” Msanii maarufu wa vichekesho nchini wa Kundi la Kashi-Kashi anayeshiriki katika kipindi cha Mizengwe cha Kituo cha ITV, Jesca Kindole (Safina) akilipigia saluti sanamu la askari wa Jeshi la Polisi wa kipindi cha kikoloni, wakati msanii huyo na wenzake walipotembelea mabanda ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.00
Wasanii maarufu wa vichekesho nchini wa Kundi la Kashi-Kashi wanaoshiriki katika kipindi cha Mizengwe kinachorushwa na Kituo cha ITV, wakichukua vipeperushi vya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi toka kwa Afisa wa Idara ya Probesheni na Huduma kwa Jamii, Pendo Mtama (kulia) wakati wasanii hao walipotembelea mabanda ya Wizara hiyo, katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Habib Mrisho (Sumaku) na Jesca Kindole (Safina).Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...